Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga(mbele
aliyesimama) akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano kuhusu
ushirikiano wa serikali na vyombo vya Habari katika kuimarisha
Mawasiliano Serikalini.Wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Maafisa Habari na
Mawasiliano leo Mkoani Tanga.
…………………………………………………………………………………………….
Na ASSAH MWAMBENE, Tanga
Baraza
la Habari Tanzania limesema kuna haja ya kujenga miundombinu
itakayoboresha ushirikiano kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari
ili kuboresha utendaji kazi katika tasnia ya habari.
Akizungumza
katika kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini
kinachoendelea mjini Tanga, Katibu Mtendaji wa MCT, Bw. Kajubi
Mukajanga amesema ili sekta ya habari iweze kuboreka ni lazima kuwe na
ushirikiano wa kutosha kati ya Maafisa Habari na Vyombo vya Habari.
Alisema
kimsingi vyombo vya habari vinatakiwa kufanya kazi kwa pomoja kutokana
na ukweli kwamba kila upande unamhitaji mwenzake ili kutimiza majukumu
yake.
“kimsingi
tunahukumiwa kufanya kazi kwa pamoja” alisema Bwana Kajubi, akinukuu
sehemu ya Hotuba aliyotoa Mhe. Rais Jakaya mrisho Kikwete katika moja ya
mikutano ya “open Government uliofanyika London Uingereza.
Akizungumza
kuhusu fikra mgando katika Vyombo vya Habari, alisema kumekuwa na
tatizo la baadhi ya wanahabari kugeuka kuwa wanaharakati na kuvaa fikra
ya kupambana na serikali kama wanavyofanya wanaharakati.
unaowaelekeza wadhani kuwa wanahabari wako katika mapambano na serikali.
“Kama
habari nzuri za serikali haziuzi mbona Timu ya Taifa au Mwakilishi wa
Taifa kwenye mashindano ya Kimataifa akishinda watu hupenda kusoma”
Alisema Bwana Kajubi.
Alisema
kwa maoni yake kushikilia kuandika matatizo tu kuhusu nchi yetu sio
kuisaidia nchi na hakujengi moyo wa wananchi kujiamini na uzalendo.
Bw.
Kajubi alikuwa akitoa mada kuhusu Ushirikiano wa serikali na Vyombo vya
habari katika kuimarisha Mawasiliano Serikalini katika kikao kazi za
Maafisa Habari na Mawasiliano. Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mkutano
wa Maafisa Habari na Mawasiliano unawahusisha Maafisa Habari na
Mawasiliano kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali,
Serikali za Mitaa, Mikoa na mashirika ya umma wapatao 130 kutoka nchi
nzima.
0 comments:
Post a Comment