ANDY CARROLL-KIFUNGO: WEST HAM YAGONGA MWAMBA!
>>RASMI KUZIKOSA MECHI 3!
West Ham, baada ya Rufaa yao kukataliwa na FA, ilitishishia kwenda Mahakamani na FA ikabidi iitishe Jopo maalum.
SOMA HABARI ZA AWALI:
ANDY CARROLL-KIFUNGO: FA YASALIMU AMRI KWA WEST HAM!
>>YAITISHA KIKAO CHA USULUHISHI KUKWEPA MAHAKAMA!
BAADA West Ham kutaka kuchukua hatua za
Kisheria, kitu ambacho hakijapata kufanyika huko England, FA imesalimu
amri na kuitisha Kikao cha Usuluhishi hii Leo Asubuhi ili kujadili
Adhabu ya Kufungiwa Mechi 3 kwa Straika Andy Carroll baada kutolewa nje
kwa Kadi Nyekundu Wikiendi iliyopita kwenye Mechi na Swansea City.
West Ham United ilitishia kuchukua hatua
za Kisheria dhidi ya FA ikiwa watakataa kumkubalia Straika wao Andy
Carroll kupewa nafasi nyingine ya kujitetea baada ya Rufaa yake kupinga
Kadi Nyekundu kutupwa nje na Jopo Huru la FA na hivyo kufungiwa Mechi 3.
Kwa mujibu wa Kanuni za FA, Chama cha Soka England, uamuzi wa Jopo Huru ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa Rufaa nyingine.
Ili kuepusha suala hili kwenda
Mahakamani, FA itakuwa na Kikao hii Leo kitakachoendeshwa na Jopo la
Watu Watatu ambapo FA na West Ham zitachagua Memba mmoja na Mwenyekiti
atakubaliwa kati yao.
Carroll alipewa Kadi hiyo Jumamosi
wakati Timu yake inaichapa Swansea City Bao 2-0 na kuonekana na Refa
Howard Webb kuwa alimpiga kipepsi Beki wa Swansea Chico Flores ingawa
marudio ya tukio hilo yalionyesha Beki huyo hakupigwa bali aliparazwa na
mkono wa Carroll juu ya kichwa waliporuka wote juu.
Kifungo hicho kitamfanya Andy Carroll
azikose Mechi 3 muhimu za West Ham ambao wanapigania kukwepa kuburutwa
kwenye vita ya kushuka Daraja.
Mechi ambazo atazikosa Carroll ni zile
na Aston Villa, huko Villa Park Siku ya Jumamosi, na zile za Nyumbani
Uwanjani Upton Park dhidi ya Norwich na Southampton.
Akiongelea ishu hii ya Carroll, mmoja wa
Wamiliki wa West Ham, David Gold, alisema wao wamelazimika kutaka
kuchukua hatua za Kisheria kwa vile hamna njia nyingine ya kufanya.
Alisema: “Hamna pa kwenda. Kilichobaki
kuchukua hatua za Kisheria. Si kitu bora sana kwani hili ni suala la
Soka. Kama tungekuwa katikati kwenye Msimamo wa Ligi pengine
tungelipuuza lakini tunapigania uhai wetu kubaki Ligi Kuu. Hapa kila
Mtangazaji wa Soka na Asilimia 80 ya Wanahabari wanasema ile sio Kadi
Nyekundu!”
0 comments:
Post a Comment