Monday, 6 January 2014

WATU 10 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA BOTI TANZANIA (ZANZIBAR)

 
Watu kumi wameripotiwa kufariki dunia na wengine hawajulikana waliko baada ya boti mbili kupigwa na dhuruba katika Bahari ya Hindi hiyo jana nchini Tanzania.
Vifo vya abiria wane vimeripotiwa kutokea mkoani Pwani baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama baharini na miili ya watu sita ni ya wale waliozama majini baada ya boti ya MV Kilimanjaro II kupigwa na dhuruba katika mkondo wa Nungwi. Boti hii ilikuwa safarini kuelekea Unguja ikitokea Bandari ya Mkoani.
Boti ya Mv Kilimanjaro II iliyokuwa imebeba abiria 380 ilipigwa na upepo mkali uliosababisha taharuki kwa wasafiri, huku watu waliokuwa wamekaa juu wakidaiwa kuteleza na kutumbukia baharini. Kundi la wazamiaji lilitumwa jana katika eneo la tukio kujaribu kutafuta watu waliozama baharini.
Ajali za boti na meli zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kuua watu wengi nchini Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.CHANZO  IRAN SWAHILI RADIO 

Related Posts:

0 comments: