Tuesday, 14 January 2014

VIFO VYA AJALI ZA MAGARI VYAPUNGUA ,VYA BODA BODA VYAONGEZEKA IRINGA


Mmoja  kati  ya  majeruhi  wa ajali za  boda boda Iringa aliyepata ajali  wakati wa mapokezi ya waziri mkuu  mstaafu Edward Lowassa mwaka  jana 
Madereva  boda boda  waliopewa mafunzo  na kamati ya  usalama barabarani mjini Iringa  wakila kiapo
Majeruhi wa bado boda  aliyevunjika mguu kwa ajili ya  bodaboda  wakati wa mkesha wa Mwaka mpya  2014 akiwa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa
Hii ni ajali ya  pikipiki iliyotokea  wakati wa mapokezi ya  Lowassa Iringa mwaka jana
Rais Dr  Jakaya  Kikwete  akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani mkoa  wa Iringa  Salim Asas kulia
Naibu  meya  wa manispaa ya  Iringa Bw Gervas Ndaki  akitazama ajali mbaya ya gari eneo la CRDB ya  Zamani mjini Iringa
Mfanyabiashara  wa  zamani Bw Makosa akiwa juu ya magari  yaliyopata ajali

 RPC Mungi  akiwa na mwenyekiti wa kamati ya  usalama barabarani Bw  Asas kulia siku  walipofunga mafunzo kwa madereva  bodaboda  mjini Iringa

.......................................................................................................................

TAKWIMU za   jeshi la  polisi mkoani  Iringa  zinaonyesha  kwa mwaka 2013  idadi ya  vifo  vya ajali  za barabarani imeshuka ukilinganisha na mwaka 2012  ambapo  watu 157 walipoteza maisha kwa ajali  za  barabarani  huku mwaka 2013  ni  watu 123 ndio   waliopoteza maisha kwa ajali  za  barabarani.

Mbali  ya takwimu  kuonyesha  kupungua kwa  vifo  vya ajali  za barabarani  zinazotokana na magari bado  kumekuwepo kwa  ongezeko la  ajali 21 za pikipiki kati ya  mwaka  2012  ambao  ulikuwa na ajali 21  huku mwaka 2013  ajali  zikifikia 42  wakati  vifo  vya  ajali  za pikipiki  zikiongezeka  kutoka 10 mwaka 2012  hadi vifo 23 mwaka 2013.

Akitoa  taarifa ya  tathimini ya ajali  kwa mwaka  2012  na 2013  wakati  akizungumza  katika mahojiano maalum mtandao  wa  www.matukiodaima.com leo  ,kamanda wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa ,Ramadhan Mungi  alisema  kuwa  ajali  za  pikipiki zimeonyesha  kuongezeka  pamoja na jitihada  kubwa  zinazofanywa na kamati ya  usalama  barabarani  mkoa  wa Iringa  chini ya mwenyekiti  wake  Salim Asas ambae  amekuwa akitoa mafunzo  ya mara kwa mara  kwa madereva  boda  boda.

Kamanda Mungi  alisema  kuwa kwa  mwaka  2012   jumla  ya makosa  ya usalama barabarani 21267 yalipatikana na mwaka 2013   makosa ya usalama barabarani  yalikuwa 28705 wakati faini  zitokanazo na makosa  hayo zilipatikana  kiasi cha  zaidi  ya Tsh milioni 6. 4 kwa  mwaka 2012  na mwaka 2013 faini  ilikusanywa  kiasi  cha zaidi ya Tsh milioni 8.9 ikiwa ni  ongezeko la zaidi ya  Tsh milioni 2.4 ukilinganisha na mwaka 2012.

 Alisema  kuwa kwa  upande wa ajali  zilizotokana na magari mbali ya watu 123 kupoteza maisha kwa mwaka  2013  bado kulikuwa na upungufu  wa majeruhi 20 ukilinganisha na  mwaka 2012 ambapo  majeruhi  walikuwa 140 na  mwaka 2013  majeruhi  walikuwa 120

Wakati  kwa ajali  zitokanazo  na pikipiki  mwaka  2012  majeruhi  walikuwa  ni 14 ila  mwaka  2013 majeruhi  wa ajali  za pikipiki  walikuwa 23 hivyo  inaonyesha ni kiasi  gari mwaka 2013  ambapo ajali  za  pikipiki  zilivyochangia  idadi kubwa ya majeruhi .

Hata   hivyo  alisema  inashangaza  kuoana  jitihada  kubwa  zinafanywa na kamati  ya  usalama barabarani katika kutoa mafunzo kwa madereva  boda  boda  ila bado ajali  kwao  zinazidi  kuongezeka  zaidi.

Kwani  alisema kwa  mwaka 2012 ni madereva 400 ndio  walipewa  mafunzo  huku mwaka 3012  jumla  ya  madereva  pikipiki 900 walipatiwa mafunzo  ya usalama barabarani  ila bado ajali  zimeongezeka  badala ya  kupungua.

Related Posts:

0 comments: