Saturday, 11 January 2014

TAARIFA MPYA KWA VYOMBO VYA HABARI (MSIBA)

Mweka Hazina wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa), Sultan Sikilo amefariki dunia na atazikwa leo katika makaburi ya Kibada, Kigamboni katika Manispaa ya Temeke.
1378039_528967223847485_1823013740_nMsiba huo umetokea kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako marehemu alikuwa amelazwa, akitokea hospitali ya Temeke ambako nako alilazwa kwa muda mfupi.
Ikumbukwe kuwa marehemu alichaguliwa miaka mitatu iliyopita na enzi za uhai wake alipitia nafasi mbali mbali katika chama ikiwa pamoja na ujumbe. Marehemu pia alikuwa Mweka Hazina wa Timu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC).

Kutokana na msiba huu, tunawaomba waandishi wa habari za michezo nchini, wadau na jamii kwa ujumla kuwa karibu na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Mungu Ailaze Roho  ya Marehemu Sultani Sikilo Peponi, Amina.
 

Majuto Omary

Mwenyekiti Taswa SC

Kwa niaba ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa)

Related Posts:

0 comments: