Saturday, 11 January 2014

MAN UNITED YAZINDUKA, YAICHAPA 2-0 SWANSEA CITY ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZA JANA

Ahead: Valencia celebrates after putting United 1-0 up just after the break at Old Trafford
Valencia akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza
Danny Welbeck akishangilia baada ya kufunga bao la pili
KOCHA David Moyes amepumua kidogo baada ya Manchester United kushinda 2-0 dhidi ya Swansea City usiku huu Uwanja wa Old Trafford na kuepuka kipigo cha nne mfululizo na cha tatu Uwanja wa nyumbani.
Ushindi wa United leo katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England umetokana na mabao ya Antonio Valencia dakika ya 47 na Dany Welebeck dakika ya 59
United sasa inatimiza pointi 37 baada ya kucheza mechi 21, ingawa inabaki nafasi ya saba kwenye msimamo
MATOKEO:
Jumamosi Januari 11
Hull 0 Chelsea 2
Cardiff 0 West Ham 2
Everton 2 Norwich 0
Fulham 1 Sunderland 4
Southampton 1 West Brom 0
Tottenham 2 Crystal Palace 0
Man Utd 2 Swansea 0

ADNAN_JANUZAJWAKIENDELEA kucheza bila Nyota wao Wayne Rooney na Robin van Persie, Manchester United jana walifanikiwa kuifunga Swansea City Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford katika Mechi ya Ligi Kuu England huku Chipukizi Adnan Januzaj akiwa Nyota kwa kusuka Bao zote mbili.
Bao hizo za Man United zilifungwa na Antonio Valencia na Danny Welbeck katika Kipindi cha Pili.
Mechi inayofuata sasa kwa Man United ni Jumapili ijayo huko Stamford Bridge dhidi ya Chelsea ambayo iko Pointi 9 mbele yao kileleni mwa Msimamo wa Ligi.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Rafael Da Silva, Smalling, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Kagawa, Fletcher, Januzaj, Welbeck.
Akiba: Giggs, Lindegaard, Hernandez, Cleverley, Buttner, Zaha, Lingard.
Swansea City: Tremmel, Rangel, Amat, Williams, Ben Davies, Britton, Canas, Pozuelo, Shelvey, Routledge, Bony.
Akiba: Taylor, Chico, Cornell, Vazquez, Richards, Donnelly, Lucas.
Refa: Chris Foy
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Januari 12
1705 Newcastle V Man City
1910 Stoke V Liverpool
Jumatatu Januari 13
2300 Aston Villa V Arsenal
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 21 21 46
2 Arsenal 20 21 45
3 Man City 20 34 44
4 Everton 21 15 41
5 Tottenham 21 1 40
6 Liverpool 20 23 39
7 Man Utd 21 11 37
8 Newcastle 20 4 33
9 Southampton 21 4 30
10 Hull 21 -5 23
11 Aston Villa 20 -6 23
12 Stoke 20 -11 22
13 Swansea 21 -4 21
14 West Brom 21 -5 21
15 Norwich 21 -18 20
16 Fulham 21 -24 19
17 West Ham 21 -10 18
18 Cardiff 21 -18 18
19 Sunderland 21 -15 17
20 Crystal Palace 21 -18 17

Related Posts:

0 comments: