HOME »
» KIPRE TCHETCHE ‘ALIVYOTUA YANGA LEO’...
MSHAMBULIAJI
Kipre Herman Tchetche leo amezima uzushi kwamba yuko kwenye mpango wa
kuhamia Yanga SC, baada ya kuibukia kwenye mazoezi ya timu yake, Azam
FC.
Nyota
huyo kutoka Ivory Coast aliwasili jana Dar es Salaam kutoka kwao
Abidjan alipokwenda kwa mapumziko baada ya msimu na asubuhi ya leo
akaibuka mazoezini Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kipre
alilakiwa na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na kuzungumza naye kwa
dakika kadhaa kabla ya kujiunga na wenzake kwa mazoezi.
|
Kipre Tchetche akikabidhiwa tuzo yake na Jemadari Said |
|
Kipre akiwasili mazoezini |
|
Anazungumza na kocha Omog |
Baadaye,
Kipre alikabidhiwa tuzo yake ya Mchezaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Meneja wa timu hiyo Jemadari Said
Kazumari.
Kipre alikuwa amekwishakwenda kwao wakati wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom Tanzania wanakabidhi tuzo za washindi mwezi uliopita.
Akizungumza
baada ya mazoezi, Kipre alisema kwamba hajawahi hata kufanya mazungumzo
na Yanga SC na anashangazwa na habari hizo. “Mimi sijawahi kuzungumza
na mtu yeyote wa Yanga, nashangaa sana,”alisema.
Baada
ya Azam FC kusajili wachezaji wawili kwa mpigo wa Yanga SC, kiungo
Frank Domayo na mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu, ikadaiwa klabu
hiyo ya Jangwani inataka kulipa kisasi kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu kwa
kuwachukua Kipre Tchetche na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Tayari
Sure Boy alikwishakanusha uvumi huo na kusema yeye ana mkataba na Azam
na kwa sasa akili yake imelalia kwenye klabu hiyo inayomilikiwa na
bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
0 comments:
Post a Comment