Mshambuliaji wa Lille ya
Ufaransa , Mkenya Divorc Origi ambaye ni raiya ya Ubelgiji aliyeifungia
Ubeljiji bao la pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika mechi yao ya
pili ya kundi H amesema kuwa anajivunia kuwa mkenya licha ya kuwa
anaiwakilisha Ubeljiji.
Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.Akizungumza na BBC Origi anasema:''aliamua kuichezea Ubeljiji baada ya kutilia maanani mambo mengi kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo, mizizi yake ya kandanda iliyoko huko, marafiki, ushauri wa babake pamoja na Ubelgiji kufuzu kwa kombe la dunia kwani haijulikani ni mwaka upi Kenya itafuzu kwa kombe la dunia.
Origi aliiambia BBC kuwa anafurahia mizazi wake na kuwa anajivunia bao hilo na familia yake iliyokuwa uwanjani kumshabikia .
Origi alisema kuwa hii ilikuwa ni tukuio spesheli kwake kwa Kenya na Ubeljiji.
0 comments:
Post a Comment