Mbeya;
Timu ya chuo cha Green hill institute ( Green hill fc)ya poteza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya wambi fc kutoka songwe. Mechi hiyo imechezwa katika viwanja vya shule ya sekondari sangu. Timu ya wambi fc ilianza kwa kasi katika kipindi cha kwanza na kufanikisha kupata goli katika dakika ya 32 likifungwa na Aliki kwa kuachia mkwaju nje ya box au nje ya kumi na nane na kumshinda golikipa na kuandikaa bao lake la kwanza.
Katika kipindi cha pili timu zilianza kwa
kasi huku kila mmoja akijaribu kuliona lango la mwenzake na katika dakika ya 57
timu ya wambi fc ilijipatia bao la pili kupitia kwa kupitia mfungaji wake Aliki.
Timu ya green hill ilishindwa kuikabili
timu ya iwambi fc kwani walielemewa na kushindwa kuliona lango la wambi fc huku
ingawa waliyofanyika mabadiliko katika dakika za mwisho ilileta matumaini kwa
timu ya green hill kwani Benzo sanga aliweza kuwasumbua mabeki wa wambi fc
lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwa hadi refali anapuliza kipyenga cha
mwisho Wambi fc 2 green hill 0.
Akizungumza na mtandao huu kapteni wa timu ya green hill fc Emanuel Daudi
amesema kiukweli mpira wa mecheza lakini bahati haikua yao Na katika mchezo kuna kushinda na kushindwa ameongeza kuwa watazidi kufanya mazoezi wala hawakati tamaa.
Na kwa upande wake Kapteni wa timu ya wambi
fc k Harifa amesema timu yao iko vizuri ndio maana wameshinda mechi hiyo na
wanarudi kwa furaha wakisubiri mchezo wa marudiano ambao utafanyika katika
uwanja wao wa wambi fc.
Baadhi ya mashabiki ya green hill institute wamesema mchezo ulikua
mzuri kwan timu zote zilipambana kwa nia ya ushindi lakini bahati ilienda
upande wa wambi fc katikamchezo huo.
Habari na Franco mkalawa
No;0754776895.
HABARI 25/06/2014
0 comments:
Post a Comment