Colombia ilikamilisha mechi zake
za makundi kwa kishindo ilipoicharaza japan mabao manne kwa moja na
kusalia kileleni mwa kundi C na alama zote 9
Timu hiyo ambayo ilikuwa imekwisha fuzu kwa
kushiriki katika mechi za timu 16 bora haikulegeza kamba kufuatia mori
ya Japan kusajili ushindi dhidi yao..Jackson Matinez alirejesha uongozi wa Colombia kabla ya kuongeza bao la tatu kwa Colombia dakika ya 82.
James Rodriguez alihakikisha Colombia imejizolea alama zote tatu katika mechi za makundi na kuwa taifa la pili kufanya hivyo baada ya Uholanzi, kwa kufunga bao la nne mnamo dakika ya 89.
Ugiriki ilifuzu kama mshindi wa pili katika kundi C na hivyo sasa itakwaruzana na washindi wa kundi D Costa Rica .
Kutokana na kichapo hicho Italia iliungana na Uingereza kama timu zilizobanduliwa nje baada ya mkondo wa kwanza .
Aidha Afrika kufikia sasa haina mwakilishi katika mkondo wa pili wa kombe la dunia .
0 comments:
Post a Comment