Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya Manyoni Mseya, akitoa taafira yake ya
ulipaji fidia kwa baadhi ya wakazi wa kijiji cha Maweni, Mwanzi na
Lusillile ili wapishe mradi wa njia ya umeme 400 KV.
HALMASHAURI
ya wilaya ya Manyoni mkoani Singida, imetumia zaidi ya shilingi 158
milioni kulipa fidia kwa baadhi ya wakazi wa vijiji vitatu,ili kupisha
zoezi la utoaji wa huduma ya umeme vijijini.
Fidia hiyo imetolewa mapema mwaka huu kwa wakazi wa vijiji vya Maweni,Mwanzi na Lusilile.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Supeet Roine
Mseya wakati akitoa taarifa yake kwa naibu wa nishati na madini Charles
Kitwanga (Mb),aliyekuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani
humo.
Amesema fidia hiyo imelipwa kwa wakazi waliokuwa eneo ambalo mradi wa njia ya umeme ya 400KV unapita.
Akifafanua,Mseya
amesema fidia hiyo imefanyika katika vijiji hivyo ambavyo havikuwemo
kwenye fidia ya kwanza iliyotolewa mwaka 2012.
“Shule
ya msingi Lusilile ambayo katika fidia ya kwanza ililipwa fidia ya
zaidi ya shilingi 3.6 milioni,uongozi wa shule hiyo ulilalamikia fidia
hiyo kuwa ni ndogo.Baada ya malalamiko hayo kufanyiwa
uchunguzi,ilibainika malalamiko hayo yana ukweli ndani yake”,amesema
Mkurugenzi huyo.
Mseya
amesema shirika la TANESCO,liliweza kuagiza shule hiyo iongezewe fidia
ya shilingi 7,442,728,lakini ilibadilisha uamuzi huona kuagiza malipo
hayo yasitishwe.
“Ofisi
yangu iliishandaa tayari hundi ya malipo hayo ya fidia ya pili kwa
uongozi wa shule ya msingi Lusilile.Sisi ni wakala tu wa TANESCO,leo hii
wakituagiza tuukabidhi uongozi wa shule ya Lusilile hundi
hiyo,tutaikabidhi haraka”,amesema Mseya.
Na Nathaniel Limu, Manyoni
0 comments:
Post a Comment