Friday, 27 June 2014

USAJILI WA WAKATA MIWA MTIBWA SUGAR MWENDIO `MDOGO MDOGO TU!



 http://www.mbwigambwiguke.com/wp-content/uploads/2013/11/mtibwa-640x360.jpg

 

WAKATA miwa wa Mtibwa Sugar wanaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji waliopendekezwa na kocha mkuu, Mzalendo, Mecky Mexime ili kurejea katika ushindani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru Lugalambwike amesema mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote wataweza kuwasainisha wachezaji ambao hakuwa tayari kuwataja.
“Kwa miaka miwili hatujafanya vizuri, msimu wa 2012/2013 tulishika nafasi ya tano. Msimu wa 2013/2014 tumeshika nafasi ya saba. Tunakiri miaka miwili klabu yetu haijafanya vizuri”. Alisema Kifaru.
“Lakini kwetu ni changamoto, tumeweza kubaini kasoro mbalimbali ambazo tunazifanyia kazi sasa, ikiwa ni pamoja na kunasa saini za wachezaji wazuri ambao wataifikisha Mtibwa katika ushindani”.
Hata hivyo, Tobias Kifaru alisema inasadikika kuna baadhi wachezaji wao Salvatory Ntebe, Juma Mpakala, Yusuf Nguya wamejiunga na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, lakini hawajui chochote.
Wakati huo huo,         Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alifafanua kuwa wamewasajili wachezaji hao watatu kutoka Mtibwa Sugar kwasababu wako huru baada ya kumaliza mikataba yao.
Bwire aliongeza kuwa Ruvu Shooting ni klabu makini na inafanya kazi kwa mapendekezo ya kocha wao Tom Alex Olaba na ndio maana waliwasainisha mikataba wachezai hao.
Bado Mtibwa wameendelea kubolewa baada ya beki wao wa kushoto Paul Ngalema kujiunga na klabu ya soka ya Ndanda fc ya Mtwara, huku beki wao wa kulia, kinda Hassan Ramadhan Kessi akiwindwa na klabu za jijini Dar es salaam
Kifaru  alisema kuwa hata mlinda mlango wao bora msimu uliopita, Hussein Sharif `Casillas` yupo kwenye rada za klabu kubwa, lakini wao hawajatangaza nani wanamuacha na nani anabaki.
Kifaru akabainisha kuwa kuna wachezaji wamemaliza mikataba na klabu hiyo, hivyo hawana tatizo nao, lakini kwa wale ambao wana mikataba, na timu nyingine zinawahitaji, basi wanasubiri mazungumzo.
 
 Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

0 comments: