R.I.P DANIEL LEMA:
R.I.P Daniel Lema
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde, mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki
cha RUCO kilichopo mkoani Iringa Daniel Lema aliyekuwa akipatiwa
matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoani Iringa baada ya kuchomwa moto
amefariki dunia.Lema aliyekuwa mwanafunzi wa kitivo cha sheria, wiki iliyopita akiwa katika maeneo ya Kihesa manispaa ya iringa alishambuliwa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto akidhaniwa kuwa ni mwizi.
Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda ni kwamba Lema alikuwa akitoka kutizama mpira/michuano ya kombe la dunia akiwa amelewa pombe majira ya saa 5 usiku katika harakati za kutafuta chakula katika migahawa ghafla mlinzi wa nyumba ya kulala wageni iliyokuwa jirani(Masai) alimhisi ni mwizi kisha kupiga kelele za kuomba msaada akidai kuwa alikuwa mwizi.
Kikundi cha watu wachache kilijitokeza na kuanza kumshambulia kwa kumpiga kisha kumwagia mafuta na kumuwasha moto wakati wakiwa katika harakati za kumpeleka polisi kisha baadhi ya wasamalia wema wakajitokeza na kuuzima moto.
Marehemu alikimbizwa katika hospitali ya mkoa ambapo alikuwa akipatiwa matibabu tangu wiki iliyopita lakini haikuwa riziki Mungu kampenda zaidi mapema mchana wa leo ameaga dunia.
Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Lema itafanyika kesho asubuhi majira ya saa moja kamili katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya iringa kisha kuanza safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayo fanyika siku ya juma tano.
Mpaka sasa mlinzi wa gest (Mmasai) aliyemsababishia kifo kijana huyo anashikiliwa na polisi mkoani iringa.
Kwa taarifa zaidi endelea kuisikiliza Ebony fm radio kutoka katika chumba cha habari ili kupata muendelezo wa ratiba ya mazishi.
Lema wakati akipatiwa matibabu katika hospitali kuu ya mkoa
Daniel Lema wa kwanza kutoka kushoto akiwa na wanafunzi wenzake enzi za uhai wake.
0 comments:
Post a Comment