DALALI (KULIA) AKIWA NA AVEVA |
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali leo ameonyesha ukomavu
mkubwa baada ya kutaka makundi ndani ya Simba yavunjike.
Dalali amewataka wanachama wote wa Simba kuungana na kuachana na masuala
ya uchaguzi.
Kabla ya kuanza kufunguka, Dalali aliwataka wanachama kuacha kumpakazia Evans Aveva kwamba aliuza gari.
Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akimsindikiza mgombea
anayemuunga mkono, Evans Aveva, Dalali alisema:
“Simba lazima iungane, hatuwezi kusema eti kuna makundi wakati lengo ni
kuleta maendeleo.
“Kama tutataka maendeleo, halafu tutakuwa na makundi, basi haina faida
ya kupata vingozi bora.
“Lazima tuungane na kuifanya Simba iwe moja ili kuleta maendeleo.
“Simba haijawa bingwa miaka mitatu sasa, si kitu kizuri na kutokuwa na umoja ndiyo lilikuwa tatizo kubwa,” alisema Dalali.
Dalali ni kati ya viongozi vipenzi vya Wanasimba kutokana na kuwa
kiongozi imara.
0 comments:
Post a Comment