KATIBU MKUU wa Yanga, Beno Njovu,
ameripotiwa kushangazwa na taarifa kuwa Straika wao Mrisho Ngassa
alikwenda Afrika Kusini kwa Majaribio na Klabu ya Free State Stars FC.
Njovu alisema kuwa walichokuwa wanajua
wao ni kuwa Free State Stars FC walionyesha nia ya kumtaka Straika huyo
mahiri na wakapewa masharti ya kumnunua.
Miongoni mwa hayo ni kutaka Klabu hiyo
ya Afrika Kusini isubiri hadi Ngassa atakaporudi Nchini, akitokea
Botswana alikotakiwa kuwepo kwenye Kambi ya Taifa Stars kama wao Yanga
walivyofikiria ndiko yuko, ili wazungumze nae kuona kama ataikubali
Klabu hiyo ili waendelee na majadiliano ya Uhamisho.
Njovu alitoboa kuwa hapo Juni 20 waliwaambia Free State Stars FC kuwa thamani ya Ngassa ni Dola 150,000.
Njovu alieleleza: “Tulichokuwa tunajua
ni kuwa Ngassa yuko na Timu ya Taifa huko Botswana na hatujui lolote
kwenda huko Afrika Kusini kufanya Majaribio na kufuzu upimwaji afya!”
‘WAPINZANI’ YANGA WAINGIA MITINI KUJIANDIKISHA!
MSEMAJI wa Klabu ya Yanga, Baraka
Kizuguto, amesema Zoezi la Kuandikisha Wanachama wao wanaopinga
Mwenyekiti Yusuf Manji kuongezewa Mwaka mmoja kwenye uongozi na ndipo
ufanyike Uchaguzi Mkuu limefungwa.
Kizuguto alisema Zoezi hizo limefungwa
baada ya Siku 5 zilizotolewa kufanywa Uandikishwaji kumalizika bila ya
‘Wapinzani’ hao kujitokeza.
Mwenyekiti Manji alipitishwa na
Wanachama 1522 kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika hivi karibuni
kuendelea kukaa madarakani kwa Mwaka mmoja zaidi na kisha ufanyike
Uchaguzi Mkuu lakini baadae kukaibuka Kikundi kilichopinga hilo.
Ndipo Manji akaamua ‘Wapinzani’ hao wajiandikishe na ikiwa watafika idadi ya 1522 basi yeye ataitisha Mkutano Mkuu wa Uchaguzi.
Kizuguto amesema suala hilo sasa
limefungwa na wao wanaelekeza nguvu zao kwenye Usajili wa Wachezaji
pamoja na maandalizi ya Msimu mpya wa Ligi unaoanza Agosti 24.
0 comments:
Post a Comment