Monday, 30 June 2014

ANGALIA: AVEVA ALIVYO SHINDA KWA KISHINDO KTK UCHAGUZI SIMBA SC

  

 10
HATIMAE Klabu ya Simba imepata Uongozi mpya baada kufanya Uchaguzi Mkuu hapo Jana huko Bwalo la Maafisa wa Polisi, Oyster Bay, Jijini Dar es Salaam.
Evans Aveva ndie aliibuka Mshindi kwa uchaguzi wa Rais kwa kumtupa Andrew Tupa kwa kuzoa Kura za kishindo 1452 dhidi ya 387 za Tupa.
Ushindi huo wa Aveva ulitangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damas Ndumbaro, ambae pia alimtaja Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kuwa Mshindi wa cheo cha Makamu wa Rais baada kuwabwaga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Swedi Nkwabi na Bundala Kabulwa.
Uchaguzi huo ulihudhuriwa na Wanachama wa Simba zaidi ya 2,000 na ulisimamiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka cha Mkoa wa Dar es Salaam [DRFA], Amin Bakhresa, huku Mbunge wa Ilala, Mussa Azan ‘Zungu’ akiwa Meza Kuu pamoja na aliekuwa Rais wa Simba, Ismail Aden Rage, Mbunge wa Tabora Mjini toka CCM.
Awali, Michael Wambura, mmoja wa Wagombea wa Urais wa Simba alieleta ‘tafrani’ ya kusababisha vuta nikuvute kati yake, Simba na TFF na hatimae kuzuiwa kushiriki, alifika hapo Bwalo la Polisi lakini akazuiwa kuingia baada kuambiwa Jina lake halipo miongoni mwa Wanachama wa Simba lakini inasemekana baadae aliruhusiwa kuingia Ukumbini.
Uchaguzi huo pia ulichagua Wajumbe Watano wa Kamati Kuu ya Simba na Majina yao tutaleta baadae.

ANGALIA PICHA JINSI WANACHAMA WA SIMBA WALIVYOPIGA KURA LEO KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA

Wanachama wa Simba wakiwa katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Klabu ya Simba katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Francis Dande)
Wagombea wa nafasi ya Urais katika Klabu ya Simba, Evans Aveva (katikati) na Andrew Tupa na wakipiga kura wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Hassan Dalali akipiga kura.
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage wakipiga kura.
 Rais wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage akiagana na mgombea wa Urais wa Simba, Evans Aveva (katikati).
 Wagombea wakitafakari.
 Wanachama wakihakiki kadi zao.
Mgombea wa Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' akizungumza na baadhi ya wanachama kabla ya uchaguzi.
Mgombea akiomba kura......Tukiwezeshwa tunaweza.
 Mgombea akijinadi.
 Mgombea wa nafasi ya Kamati ya Utendaji wa Simba, Asha Muhaji akijinadi mbele ya wapiga kura.
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiwa Rais aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
 Ibrahim Masoud Maesto akijinadi.
 Mbunge wa Mtwara, Mohamed Murji, Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu na Rais wa Simba anayemaliza muda wake, Ismail Aden Rage.
 Tunaomba kura zenu..............
 Nitaleta Maendeleo mkinichagua mimi..........................
 Simba Oyeeeeeee......................
 Jamhuri Kihwelo akielekea kujinadi kwa wanachama wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Simba.
 Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiomba kura.
 Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa, Evans Aveva.
 Wagombea wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kushoto ni Andrew Tupa (kupara), Swed Nkwabi,  Jamhuri Kihwelo 'Julio' na Evans Aveva.
 Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
  Jamhuri Kihwelo 'Julio'akimwaga sera zake.
  Jamhuri Kihwelo 'Julio'
 Kaburu akijinadi kwa wapiga kura.
Jamhuri Kihwelo 'Julio' akiteta na Evans Aveva.
 Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa.
 Evans Aveva akijadiliana jambo na Hans Pope.

 Mgombea wa nafasi ya Urais, Andrew Tupa akijinadi.
 Mgombea wa nafasi ya Urais, Evans Aveva akijinadi.
 Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Simba, Amin Bakhressa akionesha fomu za uchaguzi.
 Mmeona hakuna kitu humu....
 Asha Muhaji akipiga kura.

KABURU ' NDIYE MAKAMU WA RAIS SIMBA SC

Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC baada ya kupata kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.

0 comments: