Saturday, 28 June 2014

kocha wa Uruguay Oscar Tabarez kujiuzulu kufuatia adhabu kali

Tabarez kujiuzulu kufuatia adhabu kali dhidi ya Suarez
Kocha wa Uruguay Oscar Tabarez amesema kuwa atajiuzulu kama mwakilishi wa FIFA katika kamati mbili tofauti za kiufundi kupinga adhabu kali iliyotolewa na shirikisho hilo dhidi ya nyota wa Uruguay Luiz Suarez.
Tabarez anasema kuwa adhabu hiyo kali iliyotolewa ya marufuku ya miezi minne dhidi yake ilikuwa kisingizio tu FIFA inanjama dhidi ya Uruaguay .
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 anahudumu katika kamati mbili za kiufundi za FIFA.
Tabarez, alidai kuwa FIFA ilitoa adhabu hiyo kufuatia ushawishi wa vyombo vya habari haswa za kizungu .
Suarez anashtumiwa kumngata mlinzi wa Italia
Tabarez alikuwa akizungumza kabla ya mechi ya mkondo wa pili kati ya Uruguay na na Colombia itakayochezwa jumamosi .
Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.
FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni 65000. (£65,680).
Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.
Valcke; Suarez anahitaji matibabu
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .
Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.

0 comments: