Tuesday, 24 June 2014

KOMBE LA DUNIA: LUIS SUAREZ ‘ANG’ATA’ ANGALIA HAPA!, FIFA ITAAMUA NINI?



>>NI MARA YA TATU KUUMA MENO UWANJANI!!
CHIELLINI-ATOA-JEZISTRAIKA wa Uruguay Luis Suarez ameibua mgogoro mkubwa huko Brazil baada kuonekanaSUAREZ_AUMA_TENA2akimuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia ambayo Uruguay waliishinda Italy 1-0 na wao kutinga Raundi ya Pili.
Tukio hilo lilitokea Dakika chache kabla ya Bao la Kichwa la Dakika ya 81 la Diego Godin kuwapa ushindi Uruguay.
Mara baada ya tukio hilo la kung’atwa, Chiellini aliinua Jezi yake kumwonyesha Refa Refa Marco Rodriguez wa Mexico ambae hakuchukua hatua yeyote.
Aprili 2013, Luis Suarez alifungiwa Mechi 10 kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Mwaka 2010 huko Uholanzi, Suarez alifungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Kiungo wa PSV Eindhoven Otman Bakkal.
Miaka minne iliyopita huko Afrika Kusini kwenye Fainali za Kombe la Dunia Suarez alizuia Mpira uliokuwa ukitinga Golini kwenye Dakika ya 120 kwa Mkono wake na yeye kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, Ghana kupewa Penati ambayo Asamoah Gyan aliikosa na hatimae Uruguay kutinga Nusu Fainali kwa Mikwaju ya Penati.
SUAREZ-AMNGATA-IVANOVIC

HABARI ZA AWALI:
ITALY 0 URUGUAY 1
Italy wametupwa nje ya Kombe la Dunia na Uruguay baada ya kufungwa Bao 1-0 huku wakucheza Mtu 10 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Claudio Marchisio kwenye Dakika ya 60.
Mbali ya kufungwa na kupewa Kadi Nyekundu, hasira kubwa za Italy zipo kwa Refa Marco Rodriguez wa Mexico kwa kutoona Luis Suarez akimng’ata Meno Beki wa Italy Chiellini.
Bao la ushindi la Uruguay lilifungwa kwa Kichwa na Beki Diego Godin katika Dakika ya 81.
Toka Kundi D, Costa Rica na Uruguay zimesonga Raundi ya Pili ya Mtoano na Italy na England kutupwa nje.
VIKOSI:
ITALY: Buffon, De Sciglio, Chiellini, Darmian, Barzagli, Bonucci, Marchisio, Pirlo, Verratti, Immobile, Balotelli
URUGUAY: Muslera, Godin, Pereira, Rodriguez, Gimenez, Lodeiro, Arevalo, Gonzalez, Cavani, Caceres, Suarez
REFA: Marco RODRIGUEZ [Mexico]

0 comments: