Friday, 27 June 2014

WATU 26 WAKKAMATWA NA POLISI KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

 DSC00207
MSAKO WA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRANK MWAMPAJA (40) MKAZI WA NKUYU ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NAPOMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:46 ASUBUHI KATIKA ENEO LA ITUNGI-PORT, KATA YA BULOMA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA  KYELA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA DOUBLE PUNCH KATONI 2 NA BOSS KATONI 1. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII NA WAFANYABIASHARA KWA UJUMLA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA ZA WATU/MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 26 KWA KOSA LA KUNYWA POMBE KABLA YA MUDA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 26.06.2014 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI KATIKA MTAA WA TUKUYU – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA MSAKO MKALI ULIOFANYIKA KATIKA MAENEO HAYO.
WATUHUMIWA WOTE WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI CC 26/2014.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA ILI KUJIEPUSHA NA MATATIZO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

0 comments: