Rais wa Iran Hassan Rouhani
ameyashtumu mataifa yenye utajiri mkubwa wa mafuta katika eneo la
mashariki ya kati kwa kutumia fedha zao ili kulifadhili kundi la
wapiganaji wa kisunii nchini Iraq.
Huku akielekeza kidole chake cha lawama kwa
Saudia Arabia na Qatar ,rais Rouhani ameonya kwamba siku moja sera zao
zitawaathiri wenyewe kwa kuwa wanamgmbo hao watazigeukia nchi hizo.Akizungumza katika kongamano moja la kidini mjini Tehran ,bwana Rouhani amelalamika kuhusu tofauti inayoendelea kuibuka kati ya raia wa kishia na wenzao wa kisuni akisema kuwa hiyo ni kazi ya Israel.
Iran ndio inayoongoza kwa watu wa dhehebu la wa shia, na bwana Rouhani hapo awali amenukuliwa akisema kuwa Tehran haitasita kutetea maeneo ya makumbusho ya wa shia nchini Iraq.
Iran imekuwa ikimuunga mkono waziri mkuu wa Iraq Nouri Al Malik ambaye ni wa dhehebu la kishia.
0 comments:
Post a Comment