Shirikisho la Soka Duniani Fifa
imefutilia mbali marufuku ya miezi mitatu dhidi ya aliyekuwa kocha wa
Ujerumani Franz Beckenbauer.
Beckenbauer, ambaye ni moja kati ya wachezaji
wachache ambao wamewahi kutwaa kombe la dunia wakiwa wachezaji na pia
kama Kocha wa Ujerumani alikuwa amepigwa marufuku hiyo na FIFA kwa
kususia uchunguzi dhidi ya tuhuma za hongo zinazoiandama ushindi wa
Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mwaka wa 2022.Licha ya habari hizo nzuri Beckenbauer,hatosafiri kwenda Brazil kwa kombe la dunia ambapo timu ya ujerumani imeratibiwa kuchuana na Algeria jumatatu ijayo katika mkondo wa pili.
Beckenbauer ameshauriwa na Fifa kushirikiana na wakili mmarekani Michael Garcia anayeongoza uchunguzi huo..
Beckenbauer, ambaye ni rais wa klabu ya Bayern Munich, anasisitiza kuwa alipewa maswali ya kizungu ambayo hakuelewa mbali na kunyimwa fursa ya kujadili maswala husika kwa kina akitumia lugha yake ya Kijerumani.
Ripoti yake inatarajiwa kutolewa ifikapo mwezi Julai.
0 comments:
Post a Comment