Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
SIMBA
SC inatarajia kufanya mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu Kesho Jumapili (Juni 29
mwaka huu), katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar
es Salaam.
Kuelekea
katika mkutano huo utapata Rais mpya, makamu wa Rais na wajumbe wapya wa kamati
ya utendaji kwa mujibu wa katiba mpya Simba, mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj
Ismail Aden Rage awewatakia kila la heri wanachama wote katika uchaguzi huo.
Akizungumza
na MPENJA BLOG mchana huu, Rage amesema ana imani uchaguzi utafanyika kwa amani
na utulivu ili klabu ipige hatua.
“Nawaomba
wanachama wote hai wajitokeze ili watimize haki yao ya kidemokrasia”. Alisema
Rage.
“Nawatakia
uchaguzi mwema, nikiwa kama mwenyekiti sitakiwa kuwa upande wowote, kwahiyo
nawatakia mkutano mwema wa uchaguzi”.
“Mimi
kazi yangu itakuwa ndogo sana , kufungua mkutano na kuukabidhi mkutano kwa
kamati ya uchaguzi”. Aliongeza Rage.
Shughuli
za uhakiki wa wanachama zitaanza saa moja kamili asubuhi na Mkutano umepangwa
kuanza saa tatu kamili asubuhi na wanachama na wagombea wote wanaombwa kuwa
wamekaa katika viti vyao kufikia muda huo.
Katika
uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na Kamati ya Uchaguzi
imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa sana safari hii kutokana na ukweli
wa kuwepo kwa wagombea wengi.
Pia
Kwenye uchaguzi huo kutakuwa na huduma ya kutoa kadi kwa washabiki wa Simba
wanaotaka kuingia katika mfumo mpya wa Benki ya Posta.
Katika hatua nyingine, Rage aliwaasa wanachama na mashabiki hao kuichangia klabu hiyo kwa njia mfumo mpya walioanzisha na benki ya Posta Tanzania.
“Kwasasa
hivi tumeshirikiana na klabu ya Dar Young Africans kuingia mkataba na benki ya
Posta, nawaomba mashabiki wa Simba waliopo Tanzania nzima wapate kadi
zinazoitwa `Simba Fan Card` ili waweze kuchangia kila mwezi shilingi elfu moja”.
“Tunategemea
tukipata hela ya mashabiki angalau shilingi elfu 50 kwa mwezi, klabu yangu
itakuwa na uwezo wa kupata si chini ya milioni miatano kwa mwaka”.
“
Pesa hii itaisaidia klabu kuendeleza uwanja na kufanya shughuli nyingine za
klabu na kuifanya ijitegemee na sio kutegemea pesa za watu wachache”.
Hata
hivyo amewaomba mashabiki na wanachama kufika maeneo ya Bunju kuona maendeleo
ya ujenzi ya uwanja wa mazoezi.
“Unajua
tangu klabu hii kuanza haijawahi kuwa na kiwanja cha mazoezi, tunaazima azima
tu na nashauri viongozi watakaoingia madarakani wajue nimeacha uwanja na wao
wajenge hosteli, mahali pa kuweka wachezaji ili kupunguza gharama.”.
“Unajua
kwa mwaka tunatumia zaidi ya milioni 350 ambayo wanaweza kujenga Hosteli nzuri
kwa kiasi hicho”.
0 comments:
Post a Comment