Monday, 30 June 2014

Hofu kuwa Syria ina silaha za kemikali

Kuna hofu kuwa Syria bado inahodhi zana za maangamizi
Syria imeshindwa kutimiza makataa ya mwisho yaliyotolewa na jamii ya kimataifa kuitaka iharibu silaha zake za kemikali hivi leo.
Rais Bashar al Assad alikamilisha zoezi la kutoa silaha zilizotambuliwa rasmi juma lililopita, hii ikiwa ni miezi kadhaa baada ya siku ya mwisho iliowekwa na jamii ya kimataifa.
Bado kuna wasiwasi kwamba huenda Syria bado imehodhi zana zaidi za kinuklya.
Silaha hizo zitahariobiwa katika meli ya Marekani ya MV cape Ray katika eneo lisilojulikana ndani ya bahari ya Mediterenean.
Shughuli hiyo itachukua takriban siku sitini lakini bado kuna wasiwasi kuhusu kuwepo kwa silaha za kemikali ndani ya Syria.
Mwishoni mwa juma, usalama zaidi uliwekwa katika bandari ya Gioia Tauro nchini italy.
Vilevile vizuizi vya ukaguzi vimewekwa katika bandari hiyo.Kati ya tarehe moja na tatu mwezi July,kilomita moja ya eneo ambalo ndege hazifai kuruka litawekwa.
Makasha yaliojaa vifaa vya kutengeza silaha hatari duniani ndani ya meli moja ya Denmark Ark Futura yatafunguliwa na vifaa hivyo kuingizwa katika meli ya MV Cape Ray.
Lakini shirika la kukabiliana na silaha za kemikali duniani limekiri kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba rais Bashar Al Asaad bado anaficha vituo vya siri vya kemikali,na kuna wasiwasi zaidi kuhusu madai ya utumizi wa gesi ya klorine na wataalam wa kijeshi wameonya kuwa makundi yenye itikadi kali nchini Syria yanamiliki silaha za sumu.

0 comments: