Baadhi
ya wachezaji wa Tanzania wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu
J.K.Nyerere tayari kwa kupanda ndege kueleka nchini Scotland kwa ajili
ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya Madola.
Na Frank Shija, WHVUM
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea
Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban
Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa
katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi
waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi
wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea
uwezo wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na
wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu
walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa
kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa
bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa
wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini
Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa
kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix
amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao
iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia
walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini
Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na
kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya
Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo
wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand
0 comments:
Post a Comment