Thursday, 26 June 2014

HUYU NDIYO Gavana anaye kabiliwa na kesi ya mauaji nchini Kenya

Timamy alikamatwa Jumatano na kufikishwa mahakamani Alhamisi
Gavana wa kaunti ya Lamu Pwani ya Kenya amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa mauaji ya zaidi ya watu sitini katika eneo la mpeketoni.
Issa Timamy hata hivyo hatakiwi kujibu mashtaka hayo wakati huu.
Timamy alikamatwa Jumatano jioni na maafisa wa polisi na kuhojiwa kabla ya kuzuiliwa usiku katika kituo kimoja cha polisi. Alifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kadkalika Timamy anakuwa mwanasiasa wa kwanza wa ngazi ya juu kushtakiwa kuhusiana na mauaji hayo, ambayo ni mabaya zaidi tangu yale yaliyotokea katika eneo la Westgate Jijini Nairobi.
Walioshuhudia mauaji ya Mpeketoni walisema wanaume ndio walikuwa wanalengwa
Anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi, mauaji na kuwafnya watu kuhama makwao kwa lazima. Atasalia kizuizini hadi Juni thelathini huku uchunguzi ukiendelea. Wiki iliyopita, rais Uhuru Kenyatta alilaumu wanasiasa kwa kuchochea mauaji hayo.
Lakini kundi la Alshabab limedai kuhusika katika mashambulio hayo. Wengi wa waliofariki katika mashambulio hayo walikuwa watu wa jamii ya moja Kikuyu, kabila sawa na la rais Kenyatta.
Wakili wake na chama chake cha kisiasa kimewashutumu maafisa wa polisi kwa jinsi alivyokamatwa na kuhojiwa
Mamia ya wafuasi wa gavana huyo walifurika mahakamani kumuunga mkono gavana huyo huku baadhi ya wanasiasa wakilalamikia serikali kuhusu gavana huyo alivyokamatwa na kutendewa na polisi.
Kinpidi hiki kimekuwa kigumu kwa Kenya hasa kutokana na utovu wa usalama unaoshuhudiwa nchini
Mauaji ya Mpeketoni yalitokea tarehe 15 na 16 mwezi Juni ambapo watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito walienda nyumba hadi nyumba wakiwaua wanaume kutoka jamii moja.
Rais Uhuru Kenyatta aliwalaumu wanasiasa kwa kuwachochea wananchi kufanya mauaji hayo licha ya kundi la Al Shabaab kukiri kuyafanya.
Kenyatta alipuuza madai ya Al Shabaab , hasa kwa sababu ni watu wa kabila moja waliolengwa kwa mashambulizi hayo.
Polisi pia wamewakamata washukiwa 13 wa vuguvugu linalotaka kujitenga na Kenya na ambo wanatumuhiwa kwa mauaji hayo Mombasa.
Katika taarifa yake serikali ilisema kuwa wale waliokamatwa walikuwa wanapanga kufanya mauaji ya kikabila na kwamba walikuwa wanachama wa vuguvugu la

0 comments: