Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh.Prof Anna Tibaijuka
akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu
wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji katika Sekta ya
Nyumba.Prof.Tibaijuka alisema kuwa Serikali inaridhishwa na utendaji
unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Alisema
katika kipindi kifupi Shirika limefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya
makazi na kwamba miradi hiyo itakapokamilika,itaifanya miji hiyo kuwa
ya kisasa.Prof.Tibaijuka alisema kuwa kampuni za uwekezaji kwenye sekta
ya nyumba ni muhimu na hunyanyua uchumi wa nchi,alisema kuwa ili Taifa
liweze kuendelea ni lazima liwe na mipango miji na kwamba kupanga miji
sio kukata viwanja bali ni kunahitaji mambo mengi.Prof Tibaijuka
amewataka wananchi kuwa tayari katika suala la kupanga miji,na maeneo
yote yatakayopangwa ni lazima yafidiwe.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza mbele ya wageni waalikwa
mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye
jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba lililofanyika jijini
Dar.Bwa.Mchechu alisema kuwa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC),limedhamiria kuyabadilisha maeneo ya jiji la Dar na mikoa mingine
nchini baada ya kuzindua ujenzi wa miji midogo.
Alisema
kuwa Miradi hiyo itakapokamilika itabadilisha mandhari ya maeneo
mbalimbali nchini na kuyafanya kuwa ya kisasa,Mchechu alisema kuwa
wataanza na miradi mitatu ikiwemo miji midogo katika majiji ya Dar es
salaam na Arusha na kuendeleza nyumba zao zilizobomolewa.
Alisema
kuwa katika jiji la Dar,watakuwa na mradi wa salama Kigamboni na Kawe
mbayo italifanya jiji hilo kubadilika kuwa la kisasa,aliongea kuwa
katika miradi hiyo,kutajengwa nyumba nyingi za kuishi, biashara na
sehemu za huduma muhimu .
Mchechu
amesema kuwa mradi mwingine utakaotekelezwa ni wa Usa River Safari City
utakaojengwa jijini Arusha,ambao utalenga kulibadilisha jiji hilo na
kuwa la kisasa,aliongeza kusema kuwa mradi huo utagharimu dola za
Kimarekani bilioni mbili (zaidi ya shilingi bilioni 3.4) na itakamilika
kati ya kipindi cha miaka saba mpaka 12.Bwa.alisema kuwa miradi mingine
ambayo itatekelezwa ni pamoja na
Bagamoyo,Dodoma,Mbeya,Mtwara,Lindi,Mwanza na maeneo Mengine.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi.Zakhia Meghi akizungumza
kwa ufupi mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wakuu
wa Mikoa na Wadau mbalimbali kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya
nyumba.
Sehemu
ya meza kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye jukwaa hilo la
uwekezaji wa sekta ya Nyumba,lililofanyika jijini Dar
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kwenye jukwaa la Uwekezaji wa sekta ya nyumba.
0 comments:
Post a Comment