HOME »
» SIMBA SC YAMSAJILI CHABALALA WA KAGERA SUGAR MIAKA MITATU
KAZI
inaendelea. Simba SC imesajili mchezaji wa pili kwa ajili ya msimu
ujao, ambaye ni chipukizi wa Kagera Sugar ya Bukoba, Mohammed Hussein
Mohammed ‘Chabalala’.
Chipukizi
huyo mwenye umri wa miaka 19, anacheza beki ya kushoto na miongoni mwa
wachezaji waliong’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu
uliopita akiwa na Wakata Miwa hao wa Misenyi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameuambia mtandao huu leo kwamba, Chabalala amesaini Mkataba wa miaka mitatu.
|
Chabalala akisaini Mkataba mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC mjini Dar es Salaam leo |
“Kama
nilivyosema, tuna muda mfupi sana kwa ajili ya kufanya usajili,
tunafanyia kazi orodha ya wachezaji waliopendekezwa kwa kumalizana nao,
ndani na nje ya nchi. Baada ya Joram (Mgeveke), sasa ni
Chabalala,”alisema Poppe.
Poppe
amewahakikishia wana Simba SC kwamba safari hii watasajili wachezaji
bora ambao watarejesha heshima ya klabu hiyo msimu ujao.
Jana
Simba SC ilikamilisha usajili wa beki wa kati, Joram Mgeveke wa Lipuli
ya Iringa ambaye yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars.
Beki
huyo alicheza kwa dakika 75 mechi ya kirafiki ya Tanzania na Malawi
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo bao pekee la Amri Kiemba wa Simba
SC liliipa Taifa Stars ushindi wa 1-0 kabla ya kumpisha Kevin Yondan wa
Yanga.
Tangu
hapo, kinda huyo wa miaka 22 amekuwemo kwenye orodha ya wachezaji 18
walioshiriki mechi zote za Stars dhidi ya Zimbabwe kufuzu Mataifa ya
Afrika kama mchezaji wa akiba.
0 comments:
Post a Comment