Baadhi ya wananchi wakiangaika kutafuta maji (picha na maktaba) |
Baadhi ya wana nchi wakiangaika kutafuta maji (picha na maktaba) |
Wananchi wa mtaa wa kigamboni kata ya ramadhani wilaya ya njombe mjini mkoani njombe wameilalamikia mamlaka ya maji ya mkoa huo kutokana na kukatwa kwa maji kwa zaidi ya wiki moja sasa,
Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa mtaa huo Mzee Esau Mwafute amekili kuwapo kwa tatizo hilo na ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa mgao wa maji kumekua na tatizo la kukosa maji kwa zaidi ya wiki sasa Mwenyekiti huyo amedai kuwa awali mamlaka ilitangaza utakua na mgao kwa siku tatu katika wiki lakini matokeo yake wanakosa maji kwa zaidi ya wiki.
Kutokana na uhaba wa maji ya bomba katika mtaa huo. imewapelekea Wananchi kutumia maji ya mtoni kwa sasa,
wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu baadhi ya Wanainchi wa mtaa huo wamesema mbali na maji kuwa ni tatatizo katika mtaa wao pia wanapokea bili kubwa kuliko matumizi ya maji.
wananchi hao wamesema walisha toa malalamiko yao kwa uongozi wa idara ya maji mkoani njombe na mamlaka ikasema italifanyia kazi lakini matokeo yake utakelezaji bado mpaka leo.
kwa upande wa mamlaka ya ya maji ya mkoa huo mtandao huu hakufanikiwa kuwapata kwa kuwa simu zao zilikuwa zimefungwa
. Habari na Franco mkalawa
Njombe,
No:0754776895
0 comments:
Post a Comment