WAKATI Straika wa Argentina Sergio
Aguero akiripotiwa kuwa nje ya Kombe la Dunia, Uruguay imeazimia kukata
Rufaa FIFA kupinga Adhabu kubwa katika Historia ya Kombe la Dunia
alietandikwa nayo Straika wao Luis Suarez.
SOMA ZAIDI:
KIFUNGO MIEZI 4: LUIS SUAREZ KUKATA RUFAA!
Uruguay
imeamua kukata Rufaa kupinga Adhabu kali alizopewa Straika wao Luis
Suarez kufuatia kupatikana na hatia ya kumuuma Mebo Beki wa Italy
Giorgio Chiellini.
Rais wa FA ya Uruguay, Wilmer Valdez, amesema: “Adhabu ni kali mno kwa Faulo ile.”
Hii Leo, FIFA ilitangaza kumfungia Miezi
Minne Suarez kutoshiriki chochote kwenye Soka baada ya kupatikana hatia
na pia amefungiwa Mechi 9 za Kimataifa kuanzia Mechi ya Uruguay ya
Jumamosi ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia
zitakazomfanya awe nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Adhabu hii pia inamaanisha atazikosa Mechi 9 za kwanza za Klabu yake Liverpool za Ligi Kuu England kwa Msimu mpya.
Pamoja na Vifungo hivyo, Suarez pia ametandikwa Faini ya Dola 111,000.
SUAREZ-Adhabu zake:
-Kifungo cha Miezi Minne kwa shughuli zote za Soka ikiwa pamoja na kutoruhusiwa kukanyaga Uwanja wowote wa Soka.
-Kifungo Mechi 9 za Kimataifa
kuanzia Mechi ya Uruguay ya Jumamosi ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya
Kombe la Dunia dhidi ya Colombia
-Faini Dola 111,000
**Adhabu hizi inamaanisha atazikosa Mechi 13 za Liverpool, 9 za Ligi na nyingine 4 za Mashindano mengine.
Hata hivyo FIFA imefafanua Suarez
hazuiwi kuihama Liverpool ikiwa atataka kama inavyodaiwa kuwa huenda
akaenda Spain kuchezea ama Barcelona au Real Madrid.
Tukio hili la kumng’ata Meno Chiellini
lilitokea Juzi Jumanne kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za
Kombe la Dunia ambayo Uruguay iliifunga Italy 1-0 na kutinga Raundi ya
Pili ya Mtoano.
Hii ni mara ya 3 kwa Suarez kuadhibiwa
kwa kung’ata Meno Wapinzani kwenye Mechi na mara ya kwanza ni Mwaka 2010
huko Uholanzi, Suarez alipofungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Kiungo wa PSV
Eindhoven Otman Bakkal na mara ya pili ni Aprili 2013, alipofungiwa
Mechi 10 kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea BranislavIvanovic kwenye Mechi
ya Ligi Kuu England.
AGUERO NJE KOMBE LA DUNIA
Straika wa Argentine Sergio Aguero
atakuwa nje ya Kombe la Dunia baada kuumia kwenye Mechi dhidi ya Nigeria
waliyoshinda 3-2 hapo Jana Jumatano.
Ingawa Kambi ya Argentina huko Brazil
haijathibitisha hili, habari za kuaminika toka Mji Mkuu wa Argentina,
Buenos Aires, zimedai Straika huyo amechanika musuli Mguuni.
Kwenye Mechi na Nigeria, Aguero
alitolewa baada ya Kipindi cha Kwanza na Kocha Alejandro Sabella
alieleza ni sababu ya tatizo la Musuli.
Mechi ijayo ya Argentina ni ile ya Raundi ya Mtoano hapo Julai 1 huko Sao Paulo dhidi ya Switzerland.
0 comments:
Post a Comment