ALIEKUWA
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania anaetoka Brazil, Marcio Marcel
Maximo, ametua Jijini Dar es Salaam mbioni kujiunga na Klabu ya Yangu.
Maximo, ambae amekuja na Ndege ya
Shirika la Ndege ya Afrika Kusini, ameambatana na Msaidizi wake Leonadro
Martins Neiva na alilakiwa na umati mkubwa wa Wana Yanga.
Viongozi wa Yanga waliokwenda kumlaki waliongozwa na Katibu Mkuu, Beno Njovu.
Inatarajiwa Kesho Kocha Maximo ataongea na Wanahabari Makao Makuu ya Yanga Mitaa ya Jangwani na Twiga kuanzia Saa 5 Asubuhi.
Kuhus ujio wake Tanzania kujiunga na
klabu ya Yanga SC Maximo alisema kesho ataongea na waandishi wa habari
makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwani majira ya saa 5 kamili
asubuhi ambapo ndipo atapata fursa ya kueleza kila kitu juu ya ujio
wake.
Maximo alikuja Tanzania kwa mara ya
kwanza Mwaka 2006 kama Kocha wa Timu ya Taifa ambapo aliletwa kwa
jitihada za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na kudumu hadi 2010 na kuleta
mapinduzi na mafanikio makubwa ikiwemo kucheza Fainali za CHAN.
YANGA KESHO KUMPOKEA KIUNGO MSHAMBULIAJI MBRAZIL!!
Wakati huo huo, Yanga imetangaza kuja
kwa Kiungo Mshambuliaji kutoka Brazil Andrey Macrcel Ferreira Coutinho
ambae anategemewa kutua Kesho Saa 8 Mchana ili kujiunga na Klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment