Saturday, 28 June 2014

BRAZIL YATINGA ROBO FAINALI KWA MATUTA, CHILE YAFA KIUME


WENYEJI Brazil wameitoa Chile kwa penalti 3-2 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia mjini Uwanja wa Belo Horizonte, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Shujaa wa Brazil alikuwa ni kipa Julio Cesar aliyeokoa penalti mbili za Alexis Sanchez na Mauricio Pinilla wakati Gonzalo Jara aligongesha mwamba, huku Marcelo Diaz na Charles Aranguiz wakifunga.



Penalti za Brazil zilifungwa na David Luiz, Marcelo na Neymar, wakati Hulk  na Willian misses walikosa. Selecao sasa imetinga Robo Fainali, ambako itamenyana na mshindi kati ya Colombia na Uruguay, mchezo unaofuatia hivi sasa. Brazil ilitangulia kupata bao kupitia kwa beki David Luiz dakika ya 18 kwa kichwa baada ya kona, kabla ya kiungo Alexis Sanchez kuisawazishia Chile dakika ya 32, akimalizia pasi ya Vargas. Timu hizo zilikwenda kupumzika zikiwa zimefungana na 1-1 na kipindi cha pili, zote zilicheza kwa tahadhari, zikishambulia na kuzuia zaidi. Nyota tegemeo la Brazil, Neymar alibanwa na Wachile leo na kushindwa kufunga ndani ya dakika 120. Baada ya dakika 90, mchezo ukahamia kwenye dakika 30 za nyongeza, ambako timu hizo hazikuweza kufungana na ndipo matuta ‘yakaiteua’ Brazil kwenda Nusu Fainali. Kikosi cha Brazil kilikuwa; Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Fernandinho/Ramires dk72, Gustavo, Hulk, Oscar/Willian dk106, Neymar na Fred/Jo dk64. Chile: Bravo, Mena, Isla, Silva, Alexis, Vidal/Pinilla dk87, Vargas/Gutierrez dk56, Medel, Jara, Aranguiz na Diaz.

0 comments: