Mahakama yaruhusu uchaguzi ya Simba kufanyika juni 29 mwaka huu.
Na Baraka Mpenja, Dar
es salaam
Imechapishwa Juni 27, 2014, saa 12:58
BAADA ya mizengwe
kugubika uchaguzi wa Simba sc , sasa kimeeleweka baada ya mahakamu kuu kuruhusu
mchakato huo kuendelea kama kawaida.
Baadhi ya wanachama
wa Simba walienda mahakama kuu wakihitaji chombo hicho cha dola kusimamisha uchaguzi
wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu.
Sababu ya wanachama
hao ilikuwa ni kupinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, chini ya
mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, kuliengua jina la aliyekuwa
mgombe wa Urais, Michael Wambura kwa mara ya pili.
Hii hapa ni kauli ya
katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga aliyotoa jioni hii.
“Confirmed....
Uchaguzi upo Jumapili. Mahakama imeruhusu. Kazi kwenu wana SIMBA”.
Hata hivyo, suala la
wanachama kupelekea suala la michezo katika mahakama ya kawaida ilikuwa ni
hatari zaidi kwa klabu ya Simba kwasababu sheria za mpira ziko wazi na
hairuhusiwi kupeleka mambo ya mpira mahakama za dola.
FIFA wanataka masuala
ya mpira yasuluhishwe katika mifumo yake ya haki na si vinginevyo.
Kupeleka mambo ya
mpira mahakama za kawaida ilikuwa moja ya sababu iliyokuwa na nguvu kumuengua
Wambura kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa
vyombo vya habari na katibu mkuu wa Simba, Kamwaga jioni ya leo imesema kamati
ya Uchaguzi ya Simba SC imesema kuwa inapenda kuwaalika wanachama wote wa Simba
katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa
Jumapili, Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kamwaga alifafanua kuwa katika uchaguzi huo, jumla
ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba
suala la muda litazingatiwa sana safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa
wagombea wengi.
COUTINHO NDANI YA DAR, SASA YANGA MAMBO BOMBA!
BAADA
ya kocha mpya wa klabu ya Yanga, Mbrazil,
Marcio Maximo kuwasili jana nchini pamoja na msaidizi wake Leonadro
Martins Neiva , mchana wa leo kiungo mshambuliaji Andrey Macrcel Ferreira
Coutinho tayari yupo ndani ya Dar.
Coutinho amewasili mchana
wa leo kwa shirika la Ndege la Afrka Kusini tayari kwa ajili ya kujiunga na
kikosi cha Young Africans kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2014/2015
0 comments:
Post a Comment