Wednesday, 8 January 2014

SASA MOYES MATATANI NA FA! NA KUCHUNGUZA KAULI YAKE: ‘INACHEZA DHIDI YA MAREFA


 ’ PAMOJA NA WAPINZANI!
MOYES-MASIKITIKOFA, Chama cha Soka England, kitachunguza matamshi ya Meneja wa Manchester United David Moyes mara tu baada ya Timu yake kufungwa na Sunderland hapo Jana katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Capital One Cup.
Hiyo Jana Moyes alitamka: “Sasa inabidi tucheze dhidi ya Marefa na Timu pinzani. Ni mbaya sana. Tumeanza kuwacheka.”
Moyes alikuwa amekerwa na uamuzi wa Refa Andre Marriner kuipa Sunderland Penati iliyozaa Bao lao la Pili na vile vile kuwapa Frikiki iliyoleta Bao lao la kwanza.
Refa Andre Marriner hakuashiria Penati hiyo lakini ilibidi aitoe baada ya ushauri kutoka kwa Mshika Kibendera wake baada Adam Johnson kuanguka wakati akikabiliana na Tom Cleverley.
Kuhusu Sunderland kupewa Penati Jana, Moyes alihoji: “Itakuwaje Mshika Kibendera atoe Penati? Refa alikuwa akiangalia moja kwa moja tukio lile lakini Mshika Kibendera alikuwa haoni kwani kazibwa na Evra! Mchezaji wetu sisi alipewa Kadi kwa tukio kama hilo walilopewa Penati! Hata lile Bao la kwanza ile haikuwa Frikiki ingawa ni kosa letu kutojilinda vizuri kwa Frikiki ile na kuruhusu Bao!”
Wiki iliyopita, Moyes pia alilalamika kuhusu Marefa wakati Man United ilipofungwa na Tottenham Bao 2-1 kwenye Ligi na Refa Howard Webb kuwanyima Penati ya wazi kabisa.

0 comments: