RODGERS ASALIMU AMRI KWA FA, ANGOJA ADHABU TU!
MCHEZAJI AKIRI SHOGA
Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Germany, Thomas Hitzlsperger, amekiri kuwa yeye ni Shoga.
Hitzlsperger, mwenye Miaka 31 na ambae
amestaafu Soka Mwezi Septemba, aliichezea Germany mara 52 kati ya Miaka
ya 2004 na 2010 na pia kuzichezea Klabu za Aston Villa, VfB Stuttgart,
Lazio, West Ham United, VfL Wolfsburg na Everton.
Huku akiungwa mkono na Viongozi wa
Serikali za Germany, Hitzlsperger amedai ameamua sasa kujitokeza ili
kutetea Mashoga kwa Wanamichezo.
DOKTA AWEZA KUMPONYA WALCOTT NDANI YA MIEZI MINNE ILI ACHEZE BRAZIL!
Daktari Bingwa kutoka Scotland yupo
mbioni kuwasiliana na Arsenal ili kumuokoa Mchezaji wao Theo Walcott
kukosa kuchezea England kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil
Mwezi Juni.
Walcott, ambae aliumia Goti Jumamosi
iliyopita Arsenal walipoifunga Tottenham Bao 2-0 kwenye FA CUP,
ametangazwa kuwa atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi 6.
Lakini Profesa Gordon Mackay amedai kuwa
atatumia mbinu mpya ya kumponya Walcott ndani ya Miezi minne na hivyo
kuweza kuwahi kucheza huko Brazil.
Profesa huyo, ambae hutumia utaalam wa
kuingiza sapoti kwenye Goti na hivyo kuruhusu Mazoezi ya mapema huku
Goti likipona wenyewe, amedai ndani ya Wiki 12 Walcott ataweza kuanza
kufanya Mazoezi ya kukimbia.
Profesa Mackay ameshawahi kuwatibu
Wanamichezo kadhaa, akiwemo Mcheza Raga wa Scotland Max Evans, ambae
alirudi Uwanjani mapema mno kupita matibabu ya kawaida yanavyoruhusu.
RODGERS AKIRI KOSA KWA FA
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
amekiri kosa lake kufuatia Mashitaka yake ya kumponda vibaya Refa Lee
Mason na kusema maamuzi yake yalikuwa ya ‘kutisha’ mara baada ya
kufungwa Bao 2-0 na Man City Uwanjani Etihad Wiki iliyopita.
Sasa Rodgers itabidi asubiri adhabu yake ambayo inatarajiwa kuwa Faini.
Akiongea baada ya Mechi hiyo, Brendan
Rodgers, alisema: “Nasikia fahari kwa Wachezaji wangu. Walicheza vizuri
mno. Lakini hawakupata msaada wowote toka kwa Waamuzi. Nadhani walifanya
maamuzi ya kutisha. Hatukupata lolote toka kwao. Yule Mshika Kibendera
wa upande mmoja alishindwa kuwa mstari sawa na Wachezaji. Ukifanya kazi
hii ya kiwango cha juu ni lazima uwe na maamuzi sahihi. Ile alipewa
Ofsaidi [akimaanisha Bao la Raheem Sterling lililokataliwa] wakati si
sahihi. Ni maamuzi makubwa kwenye Mechi!”
Vile vile, Brendan Rodgers alihoji eneo
alilotoka Refa Lee Mason, ambae ni Mkazi wa Bolton, eneo ambalo liko
Maili 16 tu toka Uwanja wa Etihad na kutaka asipewe Mechi za Klabu za
Jiji la Manchester.
Alisema: “Kulikuwa na Penati ya Suarez.
Natumai hatupati tena Refa wa Eneo la Manchester katika Mechi nyingine
ya Liverpool-Manchester City!”
Baadae, Rodgers alijaribu kujitetea pale
aliposema: “Hakika sikuwa nahoji uadilifu wa Marefa. Ilikuwa ni kitu
sahihi kuuliza Refa wa eneo hilo hilo kupewa Mechi Manchester!”
Rodgers alipewa hadi leo Januari 8 Saa 3 Usiku kujibu Mashitaka hayo.
0 comments:
Post a Comment