Na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi.
Maofisa
na Askari Polisi kote nchini wametakiwa kuendelea kufanya kazi kwa
kufuata misingi na maadili ya kazi za Polisi ili kuweza kuendelea kutoa
huduma bora kwa jamii jambo ambalo litafanya mapambano ya uhalifu na
wahalifu kufanikiwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini.
Hayo
yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa akizungumza na Maofisa, Wakaguzi,
Askari na Watumishi raia ndani ya jeshi la Polisi kutoka Makao makuu ya
Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya Polisi,
kikao ambacho ni cha kwanza kuzungumza na Askari tangu ateuliwe na
Mh.Rais Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo.
Alisema
kazi za Polisi zinafanywa kwa kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa
hivyo kila Askari akifuata misingi hiyo na ushirikiano wa pamoja
ukiimarishwa mapambano dhidi ya uhalifu yatafanikiwa.
“Wananchi
wanaimani kubwa na sisi hivyo ili tuweze kuboresha uhusiano na
ushirikiano uliopo kati yetu na jamii hatuna budi kutoa huduma bora bila
upendeleo” Alisema IGP Mangu.
Kwa
Upande wake Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki alisema
muundo mpya wa utawala ndani ya Jeshi la Polisi wa kuwa na Kamisheni
mpya lengo lake ni kuboresha utendaji wa kazi za Polisi hivyo Watendaji
wa Jeshi la Polisi hawana budi kufanya kazi kwa bidii ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Aliema lengo la Muundo huo ni muendelezo wa utekelezaji wa Maboresho ya Jeshi la Polisi yanayoendelea kutekelezwa ambayo yanahitaji kufanya kazi kwa weledi, usasa na Polisi Jamii ambapo katika kipindi cha utawala wao wataendelea kuyatekeleza.
Naye
Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa alisema atahakikisha elimu ya
Polisi jamii inawafikia Wananchi wote kwa kasi kubwa ili kuendelea
kuboresha uhusiano uliopo kati ya Wananchi na Jeshi la Polisi ambapo
atahakikisha Askari Kata na Wakaguzi wa Tarafa wanafanya kazi kwa
ukaribu na wananchi ili kutokomeza uhalifu kuanzia ngazi ya familia.
MATUKIO KATIKA PICHA KIKAO CHA IGP MANGU NA WATENDAJI WALIO CHINI YAKE
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa,
Wakaguzi , Askari na watumishi raia wa Jeshi la Polisi kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya
Jeshi la Polisi (hawapo pichani) katika kikao chake cha kwanza na
watendaji hao baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.Kikao hicho
kilifanyika jana katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Ostarbay
jijini Dar es Salaam.(Kushoto) ni Naibu IGP Abdulrahman Kaniki na
(kulia) ni Kamishna wa fedha na Usafirishaji wa watu na vifaa Clodwing
Mtweve.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akizungumza na Maofisa,
Wakaguzi , Askari na watumishi raia wa Jeshi la Polisi kutoka Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na Vikosi vya
Jeshi la Polisi (hawapo pichani) katika kikao chake cha kwanza na
watendaji hao baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.Kikao hicho
kilifanyika jana katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Ostarbay
jijini Dar es Salaam.(Kushoto) ni Naibu IGP Abdulrahman Kaniki, Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja na Kamishna wa Kanda Maalumu
Suleman Kova (kulia) ni Kamishna wa fedha na Usafirishaji wa watu na
vifaa Clodwing Mtweve, DCI Issaya Mngulu na Kamishna wa Polisi Jamii
Mussa Alli Mussa.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi).
0 comments:
Post a Comment