Moyes alisema dhamira yake ni kufanya usajili wa wachezaji muhimu mwezi huo, lakini tatizo ni kwamba wachezaji anaowahitaji ni vigumu kupatikana.
Manchester United ilitupwa nje ya michuano kwa bao la dakika ya majeruhi lililofungwa na Wilfried Bony na kuifanya Swansea City kushinda 2-1 ikiwa ni mara yao ya kwanza kufanya hivyo Old Trafford baada ya miaka 83.
"Hiki ni kipindi ambacho mtu utapenda ufanye usajili wa wachezaji wapya, lakini je wachezaji tunaowahitaji wanapatikana Januari?" Alisema Moyes.
"Kuna muda nashindwa kupata jibu, kwasababu wachezaji tunaotaka waje hawapo Januari, si kwa sababu hatutaki kusajili. Nilichosema nitajaribu, lakini ukweli kuna shaka kubwa kwenye usajili wa mwezi huu."
Manchester United ilishuhudia ikipata kipigo cha tano nyumbani Old Trafford msimu huu na kuendeleza zama mbaya tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson huku kikosi hicho kikitolewa kwenye Kombe la FA ikiwa ni raundi ya tatu mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 26.
Kichapo hicho kiliwafanya mashabiki waliofika Old Trafford kuizomea timu hiyo, huku Moyes akikiri kwamba wachezaji wake ni dhaifu. Chanzo: mwanaspoti
0 comments:
Post a Comment