Baada ya kumaliza na kufanikiwa kumrudisha kocha wake, Jumma Mwambusi aliyetishia kuondoka katika klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya, klabu ya Mbeya City imefanikiwa kumsajili beki kisiki Jumma Nyoso.
Kabla ya kutua Mbeya City, Nyoso alikuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na nyingine ya ligi Kuu ya Coastal Union katika msimu iliopita .
Kusajiliwa kwa beki huyo kisiki aliyewahi kutamba na timu za Simba na Taifa stars, huenda ikasaidia kuiokoa timu hiyo na matokeo mabaya iliyoyapata tangu kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara, Septemba 20 mwaka huu.
Katika michezo saba iliyocheza kabla ya ligi kusimama imefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu na sare michezo miwili, huku ikifungwa michezo minne.
Hali hiyo ilionekana kuwakera mashabiki wa timu hiyo ambayo msimu uliopita ilipata mafanikio makubwa na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu.
Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Mussa Mapunda, amethibisha klabu yake kumsajili beki huyo na kwamba bado wanaendelea na mchakoto wa kutafuta wachezaji wengine kadhaa ingawa hakuwa tayari kuweza wazi kuwa ni akina nani na wanatoka timu gani.
Nyoso alikuwa ni mchezaji huru na tayari tumemalizana nae kama ilivyosikia na sisi tumempa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kutusaidia katika michezo iliyobaki ya ligi
alisema Mapunda.
Hata hivyo habari zilizopo zinadai kuwa klabu hiyo iko mbiuoni kumalizana na mchezaji mwingine wa kimataifa kutoka nchini Uganda na washambuliaji wawili kutoka timu kubwa zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment