Picha ya pamoja
WATANZANIA wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuweka fedha zao benki hususani Benki ya NMB kutokana na kuwa na promosheni ya Weka na ushinde ambapo wateja hujishindia Bajaji, Pikipiki na baiskeli.
Wito huo ulitolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Mbeya, Lecrisia Makiriye, alipokuwa akizungumza na wateja waliojishindia Bajaji, Pikipiki na Baiskeli kutoka Matawi ya benki hiyo mkoani Mbeya.
Makiriye alisema ni vema watanzania waendelee kuweka fedha kwenye akaunti zao ili washinde kupitia matawi ya NMB zaidi ya 160 yaliyotapakaa nchi nzima kwa kupitia mawakala wa tigo pesa na mpesa pamoja na NMB Mobile kupitia simu za mkononi.
Alisema katika Droo ya nane iliyochezeshwa nchi nzima tayari wameshapatikana washindi 34 wa bajaji, 32 wa pikipiki na washindi wa baiskeli 264 ambapo alitoa wito kwa wateja wengine kuendelea kuweka fedha kwenye akaunti zao.
Alisema kwa Kanda ya Mbeya ina jumla ya washindi 26 ambapo washindi 3 walijipatia Bajaji, washindi watatu wameshindia pikipiki na wateja 20 wamejipatia baiskeli na kuongeza kuwa zimetengwa zaidi ya shilingi Milioni 500.
|
0 comments:
Post a Comment