Sunday, 14 December 2014

ANgalia watu alio zimia jana katika mechi ya nani mtani jembe jana

 







SIMBA leo imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga katika mchezo wa Kampeni ya Nani Mtani Jembe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo kama huo Desemba 21 mwaka jana Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, yaliyofungwa na Amis Tambwe na Awadh Juma.

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Jonesia Rukyaa, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia mechi ya Simba na Yanga mwanamke kupuliza filimbi.

Mfungaji wa bao la tatu katika mchezo kama huo mwaka jana, Awadhi Juma, ndiye jana alifunga bao la kwanza dakika ya 30 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi na kutemwa na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.

Bao hilo lilionekana kuwachanganya sana wachezaji wa Yanga na kujikuta wakicheza hovyo, hali iliyosababisha wafungwe bao la pili dakika ya 40, mfungaji akiwa Elius Maguli.

Maguri alifunga bao hilo baada ya mpira wa kichwa aliopiga kugonga nguzo ya goli na kurejea uwanjani na kumkuta mfungaji aliyeukwamisha wavuni na kumuacha Dida akigaagaa.

Yanga ingeweza kupata bao la mapema kutokana na kufanya mashambulizi ya kushtukiza baada ya kuanza mchezo huo, lakini umalizijia haukuwa mzuri.

Mshambuliaji mpya wa Yanga, raia wa Liberia, Kpah Sherman mara kadhaa alijaribu kufurukuta lakini alikosa ushirikiano wa kutosha.


Simba nayo licha ya ushindi huo, lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Simon Sserunkuma, Elias Maguli na Emmanuel Okwi walipata nafasi za kufunga, lakini walishikwa na kigugumizi cha miguu kila waliposogea eneo la hatari.

Kipindi cha pili, Yanga ilipata pigo baada ya Sherman kuumia, hivyo kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa.

Dakika ya 62, Danny Mrwanda aliyeingia kipindi cha pili badala ya Andrey Coutinho nusura aipatie Yanga bao, baada ya mpira aliopiga kuokolewa na beki Hassan Isihaka, wakati kipa Ivo Mapunda hayupo golini.

Dakika ya 67 Sserunkuma akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, shuti lake lilipaa juu kidogo ya lango la Yanga, huku tayari baadhi ya mashabiki wa Simba wakianza kuinuka wakiamini amefunga.

Simba: Ivo Mapunda, Nassor Masoud, Mohammed Hussein/Issa Rashid,
Hassan Isihaka,  Juuko Murishid/Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Said Ndemla, Awadh Juma, Elius Maguri/Danny Sserunkuma, Simon Sserunkuma/Shaaban Kisiga na Emmanuel Okwi.

Yanga: Deogratius Munishi, Abdul Juma/Hussein Javu,Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite/Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Emerson Roque/Salum Telela, Simon Msuva, Kpah Sherman/Mrisho Ngassa na  Andrey Coutinho/Danny Mrwanda.

0 comments: