MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hanspope amesema kikosi cha Yanga SC walichokichapa mabao 2-0 jana ni kibovu, hivyo wana kazi ya ziada kuhakikisha wanakuwa na timu imara zaidi.
Simba SC iliifunga Yanga SC mabao 2-0 katika mechi ya Nani Mtani Jembe 2 iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana jioni. Shukrani kwa mabao ya kiungo Awadh Juma na mshambuliaji Elias Maguri waliyoyafunga kipindi cha kwanza.
Hanspope ameuambia mtandao huu kuwa kikosi cha Simba SC kilicheza vizuri lakini hawapaswi kubweteka kwa sababu wamepata ushindi na kucheza soka zuri dhidi ya timu iliyokuwa mbovu ya Yanga SC.
“Tulicheza vizuri lakini tulicheza na timu mbovu. Yanga hawako vizuri, tungepata ushindi dhidi ya timu bora tungejivunia. Zipo timu nzuri msimu huu kama Mtibwa Sugar na si Yanga hawa wabovu,” amesema Hanspope.”
Sisi (Friends of Simba) tumechukua timu ili tuipe mafanikio, hatujachukua timu ili tuiharibu. Tunawaomba wanasimba watupe muda na watuamini tuitengeneze hii timu,” amesema zaidi Hanspope.
Yanga SC pia ilifungwa mabao 3-1 na Simba SC katika mechi ya kwanza ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 21 na kupelekea kufukuzwa kwa benchi zima la ufundi la Yanga.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na mshambuliaji Mrundi Amissi Tambwe aliyefunga mara mbili na kiungo Awadh ambaye ameweka rekodi ya kufunga katika mechi ya Nani Mtani Jembe. Bao pekee la Yanga SC lilifungwa na mshambuliaji Emanuel Okwi ambaye hata hivyo amerudi katika timu yake ya Simba SC.

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
0 comments:
Post a Comment