Saturday, 13 December 2014

LIGI KUU ENGLAND LEO ARSENAL NA NEWCASTLE NANI MSHINDI?

 

MENEJA wa Newcastle Alan Pardew ndie ameteuliwa Meneja Bora wa Ligi Kuu England kwa Mwezi Novemba na Mchezaji Bora ni Sergio Aguero wa Manchester City.
Alan Pardew, mweye Miaka 53, alishinda Mechi 3 kati ya 4 na kuwabwaga Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, na Manuel Pellegrini wa Man City ambao hawakufungwa hata Mechi moja.
Hivyo hivyo, Sergio Aguero amepewa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wakati Mchezaji wa QPR, Charlie Austin, na wa Burnley Danny Ings walifunga Bao 3 kama Aguero ambae hii itakuwa Tuzo yake ya Pili.

TUZO YA UBORA KWA MWEZI-WALIOTWAA MARA NYINGI:
-Sir Alex Ferguson – Mara 27 [Man United]
-Steve Gerrard­ - 6

Ligi Kuu England inaendelea Leo hii kwa Mechi 7.
 Saa za Bongo
Jumamosi Desemba 13
1800 Burnley v Southampton               
1800 Chelsea v Hull City   
1800 Crystal Palace v Stoke                 
1800 Leicester v Man City          
1800 Sunderland v West Ham               
1800 West Brom v Aston Villa              
2030 Arsenal v Newcastle 
Jumapili Desemba 14
1630 Man United v Liverpool                
1900 Swansea v Tottenham        
Jumatatu Desemba 15
2300 Everton v QPR         

0 comments: