Monday, 15 December 2014

TAMBWE AITWA NA VITAL'O BAADA YA SIMBA KUMTUPIA VIRAGO,



Baada ya Simba kumtema, mshambuliaji Amissi Tambwe anaanza kujiandaa kurejea kwao Burundi.

Tambwe amemuambia rafiki wake wa karibu kwamba anarejea na kujiunga na timu yake ya zamani ya Viral’O.

“Amesema Vital’O wamemuita, hivyo anachosubiri ni kumalizana na Simba kuhusiana na haki zake,” alisema rafiki huyo wa Tambwe.


Tambwe alitokea Vital'O na kujiunga na Simba, wakati akiichezea timu hiyo ya Burundi alikuwa mfungaji bora wa Burundi pia michuano ya Cecafa.

Lakini alipoulizwa Tambwe akasema atazungumza baadaye kidogo kwa kuwa kuna watu anataka kumalizana nao. Sijui ni akina nani?

0 comments: