Serikali kupitia idara ya afya katika Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya imetoa kiasi ya cha sh. 4000000/= kwa ajili ya ujezi wa zahanati ya Matamba ambayo inaendelea kujengwa kwa nguvu za wananchi.
Akizungumza na mwandishi wetu mganga mkuu wa Harimashauri ya wilaya ya Busokelo wilayani humo Gibert Tarimo alisema kutokana na wananchi wa kijiji hicho kuonyesha moyo katika ujenzi wa zahanati yao baada ya kusumbuka kwa muda mrefu katika kutafuta huduma ya matibabu, serikali kupitia bidala hiyo imetoa shiringi milioni nne kwa ajili ya kusadia kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo.
“ Serikali kupitia idara ya afya iliona ni vyema ikashirikiana na wananchi wa kijiji hiki katika ujenzi wa kituo chao cha afya kwakuwapatia msaada wa pesa kiasi cha shilingi milioni nne ambazo zitatumika kumalizia ujenzi wa zahanati hii
Adha Tarimo aliwataka wanachi kuendelea na moyo huo na kusema kufanikisha kwa kazi hiyo kuta tegemea na uelekezi wa nguvu zao katika ujenzi wa zahanati hiyo.
Jampyoni mbuguru ambaye ni mwanachi wa kijiji hicho mbali na kuupongeza uongozi huo kwa jitihada walizo zionesha alisema uwepo wa kituo hicho utasaidia wao kupunguza vifo vya watoto na ndugu zao ambao walikuwa wakipatwa na maafa wakati wa kuwakimbiza katika vituo vya afya .
“ sisi kama wananchi tuliamua kuanza ujenzi wa kituo hiki baada ya kutembea umbali mrefu katika kutafuta huduma muhimu ya afya ambayo inapatika zaidi ya kilometa {7} na kusema wakati mwingine ndugu zetu wamekuwa wakifia njiani pindi tunapowapeleka katika vituo hivyo kwa matibabu zaidi na ukizingatia kuwa katika maeneo haya hakuna usafiri zaidi ya baisikeli”. alisema Mbunguru.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Johan mwakyoma kwa upande wake alisema katika kukamilisha hatua hiyo walijipangia kutoa kiasi cha shiringi elfu thelatini kwa kila mmoja 30000/= ambazo wanazitoa kwa awamu sita na kusema mpaka sasa wamemaliza hatua ya linta na wamenza ufyatuaji wa tofari na kuwalipa mafundi.
Na, Baraka lusajo Rungwe
0 comments:
Post a Comment