Tuesday, 2 December 2014

CHADEMA YASEMA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WAADILIFU




Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Mbeya mjini John Mwambigija aliyesimama katikati aliyevaa kofia upande wa kulia ni Samweli Ndoni Mwandishi wa habari wa Highlands fm

 Baadhi ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza mwenyekitti huyo kwa wakati akifanya uzinduzi huo



Baadhi ya wananchi wakimshangilia  mwenyekiti huyo wakati wa uzinduzi.


Chama cha demokrasia na maendeleo mkoani mbeya  kimewataka wananchi kuacha  dhana ya kuamini kuwa vyama vyote vya siasa ni viadilifu na vinalengo moja la kuwatumikia  wananchi kulingana na sera ya chama husika.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mbeya mjini  John Mwambigija alipokuwa akizungumza na mtandao huu katika uzindua wa kampeni za uchaguzi wa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa katika kitongoji cha ilongoboto kijiji cha mpandapanda kata ya kiwira wilaya ya rungwe mkoani mbeya.
\
Mwambigija amesema chama cha Chadema kimekuwa na uwezo wa kuwawajibisha viongozi wake wanaokwenda kinyume na sera ya chama, tofauti na vyama vingine vimekuwa vikiwakumbatia viongozi wake ambao si waadilifu.

Aidha Mwambigija amesema dhana ya wananchi kuamini kuwa wanapaswa kuchagu mtu na si chama ni kujinyima haki hao ya mingi. “wananchi wanatakiwa kuchagua chama chenye uwezo wa kuwawajibisha viongozi wake ambao si waadilifu kwakufanya hivyo watakuwa wamepata haki yao ya msingi, mimi nawaambia wananchi wa kijiji cha mpandapanda na Taifa kwa ujumla kama mtachagua viongozi wa vyama vuinavyo wakumbatia viongozi wanaokula kodi yenu kisha wanawakatetea basi mtaendelea kuchangishwa michango isiokuwa na tija kila wakati” alisema Mwambigija.

Hata hivyo Mwambigija amesema chama cha Mapinduzi CCM kimekuwa ni moja kati ya vyama vinavyowakumbatia viongozi wake ambao ni mafisadi ikiwa wanafahamu wazi kuwa viongozi wake wanakula kodi za wananchi pasipo huruma yeyote.

Akitolea mfano wa sakata la fedha shilingi bil. 321 zilizoibiwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kwamba viongozi wa CCM ndio wahusika wakubwa lakini jambo la kushangaza tuhuma hizo zimefunikwa funikwa bila majibu sahii hivyo inaonesha kuwa chama hicho kinashindwa kuwawajibisha viongozi wake.

0 comments: