Thursday, 4 December 2014

UJENZI MAABARA WA ENDELEA Mkoa wa Arusha Umetekeleza agizo la raisi

maabara

Mkoa wa Arusha Umetekeleza agizo la raisi la ujenzi wa maabara kwa asilimia 80% hadi Novemba 30 mwaka huu ambapo hadi kufikia desemba,10 watakuwa wamekamilisha kwa asilimia 90% ya ujenzi huo.

Hayo yalibainishwa na Katibu tawala msaidizi wa mipango na uratibu Anza Amen Ndossa ofisini kwake wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa wilaya ya Karatu ilikuwa nyuma katika uhamasishaji kutokana na malumbano ya kisiasa.
Ndosa alisema kuwa mkoa wa Arusha unajumla ya shule 138 za sekondari za serikali ambapo mahitaji ya vyumba vya maabara ni 414 ambapo vilivyokamilika ni 105 sawa na asilimia 25% huku ambavyo vipo katika hatua mbalimbali ya ukamilishaji ujenzi na uwekaji wa vifaa ni 309 .
Alibainisha kuwa Halmashauri ya jiji la Arusha ndio inaongoza ikiwa na shule 24 huku mahitaji ya vyumba vya maabara ni 72 ambapo vilivyokamilika ni 15 huku 57 vipo katika hatua mbali mbali za ukamilishaji.
Ndossa,alisema kuwa wilaya ya Ngorongoro ina jumla ya shule 10 huku mahitaji ni vyumba 30 vilivyokamilika 12 huku 18 vipo kwenye hatua mbali mbali za ukamilishaji.
Alisema kuwa wilaya ya Longido inajumla ya sekondari 7 mahitaji ni vyumba 21 vilivyokamilika ni 3 huku 18 vipo kwenye hatua mbali mbali za ukamilishaji
Aliendelea kusema kuwa Halmashauri ya Arusha DC, ina Sekondari 26 mahitaji ni vyumba 78 vilivyokamilka 23 huku 55 vipo katika hatua mbali mbali,wilaya ya Monduli ina sekondari 13 mahitaji ni vyumba 39 vilivyokamilika ni 15 huku bado24 vipo katika hatua mbalimbali.
Karatu sekondari 29 mahitaji 87 vilivyokamilika11 huku 76 vikiwa katika hatua mbali mbali za ukamilishaji,akamalizia na halmashauri ya Meru ina sekondari 29 mahitaji ni 87 huku 26 vikiwa vimekamilika na vilivyo kwenye hatua ya ukamilishaji ni 61.
Ndossa,alisema kuwa ziara aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, aliyoifanya Oktoba 15 mwaka huu imesaidia kubadilisha mitizamo ya wananchi wa Karatu na kuamua kuitikia wito wa kuchangia ujenzi wa maabara ambao awali walikuwa wakisuasua kutokana na siasa .
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa alikutana na baraza la madiwani pia wananchi na kuwaeleza kuwa swala la ujenzi wa maabara sio swala la chama bali ni swala la maendeleo na hivyo watoto watakaoshindwa kufanya mazoezi na mitihani ya sayansi kutokana na ukosefu wa maabara ni wao hivyo ni jukumu lao kuchangamkia ujenzi huo wa maabara.
“Ujenzi wa maabara umeathiriwa na ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wahamasishaji wakubwa wa maendeleo ambao ni wenyeviti wameingia kwenye kampeni za uchanguzi hivyo ushiriki wao kwenye kuhamsisha ujenzi wa maabara unakuwa ni mgumu’’alisema Ndossa..
Ndossa,alisema kuwa wananchi wamepata mwamko wa uchangiaji baada ya ziara hiyo ya mkuu wa mkoa,japo zoezi hilo limegongana na uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji ambapo wenyeviti wa vijiji ndio wasimamizi wa uhamasishaji na ukusanyaji wa michango ya ujenzi huo.
Alisema kuwa wananchi wamepata mwamko wa uchangiaji japo zoezi hilo liligongana na uchaguzi wa serikali za mitaa,vitongoji na vijiji ambapo wenyeviti wa vijiji ndio wasimamizi wa uhamasishaji na ukusanyaji wa michango ya ujenzi huo.
Aliongeza kuwa ifakapo Desemba 9 mwaka huu wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru mikoa na wilaya zitatakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la rais kuhusu ujenzi wa maabara katika shule zote za sekondari nchini

 

0 comments: