Monday, 8 December 2014

AZAM FC KUCHAPANA NA MTIBWA LEO USIKU KABLA YA KUPAA UGANDA

azam
Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzanika Bara (VPL), Azam FC kesho Jumanne usiku kitashuka Uwanja wa Azam jijini Dar es Salaam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wabaya wa Simba, Mtibwa Sugar.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd Maganga amesema jijini hapa leo kuwa kikosi chao kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kitashuka Azam Complex saa moja usiku kumenyana na wakatamiwa hao ambao msimu huu wameonesha kuwa ni moto wa kuotea mbali wakiongoza msimamo wa VPL wakiwa na pointi 15, mbili mbele ya Azam FC na Yanga SC walioko nafasi za pili na tatu.
Mtibwa inayonolewa na Mecky Mexime, ilikipa kipigo cha bila huruma cha mabao 4-2 kikosi cha Simba SC jana jioni kwenye Uwanja wa Azam.
aza
Baada ya mechi ya kesho, Maganga amesema watapaa kwenda Uganda kucheza mecjhi za kimataifa za kirafiki dhidi ya timu za Ligi Kuu ya nchini humo zikiwamo KCCA na SC Villa iliyomkuza mshambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba SC.
“Tucheza mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar FC kesho Jumanne usiku, uwanja wetu una taa hivyo tumeona mechi ichezwe usiku ili kuwapa nafasi watu kusishudia baada ya sherehe za maadhimisho ya Miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania.
“Viingilio vitakuwa Sh. 2,000 na 1,000. Baada ya hapo kikosi chetu kitakwenda Uganda kucheza mechi za kimataifa za kirafiki kabla ya kurejea nchini kuendelea na Ligi Kuu ya Vodacom,” amaesema Maganga.
Mtibwa FC itakuwa na faida ya kuuzoea Uwanja wa Azam kwani itachuana na Azam FC katika mechi inayofuata ya raundi ya nane ya VPL msimu huu kwenye uwanja huo huo

0 comments: