BAADA ya kuichapa Stoke City Jumanne iliyopita na huo ukiwa ushindi wao wa 4 mfululizo kwenye Ligi Kuu England, Jumatatu Usiku Manchester United wanasafiri kwenda huko Uwanja wa Saint Mary kucheza na Southampton ambayo iko Nafasi ya 3 na wakishinda watatwaa wao Nafasi ya 3.
Lakini Southampton, chini ya Ronald Koeman ambae ashawahi kukorofishana na Meneja wa Man United Louis van Gaal wote walipokuwa Ajax Mwaka 2009, si Timu ya kubeza.
Hata hivyo, katika Mechi zao mbili zilizopita Southampton wamepata vichapo viwili mfululizo toka kwa Manchester City na Arsenal.
DONDOO MUHIMU:
-Man United wameshinda Mechi 21 kati ya 30 za Ligi Kuu England dhidi ya Southampton na mara ya mwisho kufungwa nao ni Agosti 2003.
Hali za Timu
Nahodha wa Man United Wayne Rooney atarejea Uwanjani baada ya kuumia Goti Jumamosi iliyopita walipocheza na Hull City na kuikosa Mechi na Stoke City.
Hata hivyo, United itamkosa Winga wao kutoka Argentina Angel Di Maria ambae ana tatizo la Musuli za Pajani [Hamstring].
Majeruhi wengine wa Man United niDaley Blind na Phil Jones ambao ndio kwanza wameanza Mazoezi na hawatakuwa fiti kwa Mechi hii.
Southampton watamkosa Beki wao mahiri Toby Alderweireld pamoja na Morgan Schneiderlin na Jack Cork ambao ni majeruhi.
Akiongelea Mechi hii, Van Gaal amesema: "Tupo kwenye hali nzuri. Tumeshinda Mechi 4 mfululizo na hiki ni kitu chema kwenye Ligi Kuu. Tukishinda Mechi hii, ya Pili Ugenini, tutakuwa kwenye msukumo mzuri!”
Mechi ya mwisho kati yao
Ilikuwa ni Mwezi Mei Uwanjani Saint Mary katika Mechi ya mwisho ya Msimu uliopita na kutoka Sare 1-1.
Rickie Lambert aliipa Bao Southampton katika Kipindi cha Kwanza na Frikiki safi ya Juan Mata katika Dakika ya 54 iliwapa Bao la kusawazisha Man United.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Southampton: Forster; Clyne, Fonte, Yoshida, Bertrand, S Davis, Wanyama, Reed, Long, Pelle, Mane
Manchester United: De Gea; Valencia, Smalling, Rojo, Young, Herrera, Carrick, Fellaini, Rooney, Van Persie, Wilson
REFA: Kevin Friend
0 comments:
Post a Comment