Jana December 14 kwenye Historia ya mwaka 2014, Mashindano makubwa ya Miss World 2014yalikuwa yakifanyika London, Uingereza ambapo washiriki mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwakilishi wa Tanzania, Happiness Watimanywa akiwa mmoja ya washiriki hao.
Mpaka leo asubuhi matokeo ya kura ambazo zilikuwa zikipigwa na watu zilimuweka mwakilishi huyo kuwa katika nafasi ya pili, akitanguliwa na Miss Thailand ambapo iwapo Happiness angekuwa namba moja basi ilikuwa moja kwa moja aingie kwenye Top 10 ya mashindano hayo.
Kutokana na Hapiness kupitwa kura na Miss Thailand hakufanikiwa kuingia kwenye Top 10, huku katika wale waliotajwa ni wawakilishi wawili pekee, mmoja wa South Africa na mwakilishi wa Kenya waliofanikiwa kuingia Top 10.
Mwakilishi wa South Africa, Rolene Strauss amefanikiwa kuvuka hatua zote na hatimaye kutangazwa mshindi wa Taji la Miss World 2014, nafasi ya pili ikishikwa na Miss Hungary, Edina Kulcsar na nafasi ya tatu kushikwa na Miss USA, Elizabeth Safrit.
Hapa nimekuwekea picha za matukio yote ya sherehe hizo.
0 comments:
Post a Comment