Yacine Brahimi akiwa na tuzo yake ya BBC.
MSHINDI wa tuzo ya BBC ya mchezaji bora wa mwaka 2014 Afrika imekwenda kwa mchezaji wa Algeria na nyota wa Porto, Yacine Brahimi.
Hapajawahi kutokea katika miaka 23 ya historia ya shindano hilo kwa mchezaji bora kutoka Algeria kuishinda tuzo hiyo, lakini Brahimi amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka uliokuwa na mbwembwe nyingi.
Brahimi amewabwaga wachezaji wengine nyota wakiwemo, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon, Vincent Enyeama wa Nigeria, Gervinho wa Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment