Saturday, 6 December 2014

WAPOFUKA MACHO BAADA YA KUFANYIWA OPERATION


Maafisa wa utawala nchini Indiaa wanafanya uchunguzi kufuatia madai ya wagonjwa 15 kupofuka baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutibu ugonjwa ujulikanao kama ''mtoto wa Macho' au Cataract bila malipo.


Upasuaji huo ulikuwa unafanywa na shirika moja lisilo la kiserikali katika kambi iliyotengewa matibabu hayo.

Maafisa wakuu wanasema kua kambi ambako upausuaji huo ulifanyika haikuwa na idhini inayostahili na pia waliokua wanaufanya upasuaji huo hawakuwa na vifaa vinavyostahili.

Lakini tajiri mmoja ambaye alifadhili mradhi huo, alisema wagonjwa wote 49 wa macho waliofanyiwa upasuaji walipewa huduma nzuri.

Mfumo wa afya nchini India uko chini ya darubini hasa baada ya wanawake 15 kufariki baada ya kufanyiwa upasuaji wa kufungwa kizazi.

Maelfu ya watu hufanyiwa upasuaji wa kuwatoa 'Cataract ' kwenye macho kila mwaka katika kambi za matibabu na hospitali za serikali.

Upasuaji huo kwa kawaida huonekana kuwa rahisi sana kufanywa.

Kufuatia matibabu hayo, takriban wagonjwa 15 wanasema hawajaweza kuona tena.

Madaktari katika hospitali ambako wagonjwa 11 wamepelkwa kwa martibabu wanasema wagonjwa sita au saba hawataweza kuona tena.

Mmoja wa madaktari hao, Karamjit Singh aliambia vyombo vya habari kuwa watu hao wana ugonjwa wa macho.

Aliongeza kusema kuwa ugonjwa huo umeenea hadi katika sehemu nyinginezo za macho na kwamba ityakuwa vigumu kwao kuweza kuona tena.

0 comments: